WAZIRI UMMY AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA WHO NCHINI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo tarehe 6 Julai 2023 amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Charles Sagoe-Moses kwa pamoja wamefanya mapitio shirikishi ili kuangalia hali ya utekelezaji wa Afya kwa wote na utayari wa kukabiliana na magonjwa ya dharura ikiwemo magonjwa ya milipuko nchini (Universal Health and Preparedness Review - UHPR).


Katika Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Afya Jijini Dodoma, Waziri Ummy amesema iundwe kamati ambayo itashiriki maandalizi ya ripoti na baada ya kuridhiwa itafikishwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuizindua kwa ajili ya utekelezaji. 


Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Tanzania Dkt. Charles Sagoe-Moses amesema Shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania hasa katika kukabiliana na magonjwa ya Milipuko.

“Tutaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania na hasa katika kuliendea hili la mapitio shirikishi ili kuangalia hali ya utekelezaji wa Afya kwa wote na utayari wa kukabiliana na magonjwa ya dharura nchini”. Amesema Dkt. Sagoe-Moses.


Kikao hicho kimeandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kumpitisha Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.






Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)