WAZIRI KAIRUKI AKABIDHIWA MIRADI YA BILIONI 1. 1 NA WORLD VISION WILAYANI KOROGWE.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe. Angellah Kairuki amezindua vyumba vya madarasa na kupokea miradi iliyotekelezwa kwa ufadhili kwa Shirika la World Vision katika Halmashauri ya Wilaya Korongwe yenye Jumla ya takribani bilioni 1.1 ambayo inawanufaisha Wananchi zaidi ya 13,700.


Waziri amezindua na kupokea miradi hiyo tarehe 06 Julai 2023 iliyotekelezwa katika Kata za Mnyuzi na Kwagunda  wilaya ya Korogwe mkoani Tanga katika sekta ya Elimu, afya na Maji.


Waziri Kairuki amekagua na kuzindua Vyumba 8 vya madarasa na ofisi ya walimu, ikiwa ni pamoja na madawati 300, nyumba ya watumishi yenye uwezo wa kuchukua familia 2 na Matundu 48 ya vyoo kwa ajili ya Wanafunzi.


Aidha, amekagua Upanuzi wa Zahanati ya Mnyuzi kwa kujengwa jengo la la Wagonjwa wa Nje (OPD) pamoja na huduma ya Mama na Mtoto, nyumba ya wataalam wa afya, Vifaa tiba  na choo kwa ajili ya matumizi ya Wagonjwa.

Wakati akikabidhiwa Miradi hiyo, Waziri Kairuki kwa niaba ya Serikali amelishukuru Shirika la World Vision Tanzania kwa kuunga Mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha maisha ya Watoto, familia na Jamii kwa ujumla.


Waziri Kairuki ametumianafasi hiyo kuelezea kazi iliyofanywa na Serikali, amesema katika maka wa fedha wa 2022/23 zaidi ya shilingi milioni 121.1 ambazo zilielekezwa katika miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu katika mkoa wa Tanga.


Amesema Serikali ilitoa shilingi milioni 584 kujenga shule Mpya ya Sekondari katika kata ya foroforo,  shilingi milioni 260 zilipalekwa shule ya Sekondari Mnyuzi na Magoma kujenga mabweni vilevile shilingi milioni 699 zilimetolewa kupitia Mradi wa BOOST kuboresha miundombinu ya madarasa na kujenga shule mpya.

Katika Sekta ya Miundombinu, Waziri Kairuki amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/24 Serikali imetenga Shilingi Bilioni 37 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara kupitia TARURA katika Mkoa wa Tanga.


Kadhalika, Katika Sekta ya ya Afya amesema Serikali itatoa milioni 150 kukamilisha Zahanati ya Mnyuzi.


Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa World Vision Tanzania, James Angawa amesema Shirika hilo litaendelea kuwa msatari wa mbele kushirikiana na Serikali kuleta Maendeleo kwa Watanzania na wamepanga kuwafikia watoto milioni 3.2 wanaoishi katika Mazingira magnum katika lipidi cha mica miwili.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)