WADAU WA MADINI WARIDHISHWA NA ELIMU KUTOKA TUME YA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Wadau mbalimbali wanaotembelea  Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam wameipongeza Tume ya Madini kwa elimu iliyokuwa inatolewa na watalaam wake na kuomba elimu kuendelea kutolewa katika mikoa yote nchini ili kuongeza ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini.


Wadau hao wameyasema hayo mapema leo Julai 11, 2023 mara baada ya kupata elimu kuhusu fursa zilizopo katika Sekta ya  Madini, namna ya kutuma maombi ya leseni mbalimbali za madini, biashara ya madini na usimamizi wa afya na mazingira  kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.


"Tunaiomba Tume ya Madini kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika mikoa yote kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana katika Sekta  ya Madini na namna ya kushiriki ili mbali na mchango wa Sekta ya Madini kuongezeka kwenye Pato la Taifa, mwananchi mmoja mmoja anufaike, " wamesema wadau hao.






Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)