MAPATO YA STENDI YA MAGUFULI YAFIKIA MIL 5 KWA SIKU.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Mapato ya viingilio katika kituo kikuu cha mabasi yanayowenda mikoani na nje ya nchi kilichopo Mbezi kilichopewa jina la Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Magufuli, Dar es Salaam yameongezeka kutoka Sh 3, 400,000 kwa siku hadi Sh 5,6 00,000.


Meneja wa kituo hiko, Isihaka Waziri alisema ongezeko hilo ni matunda ya udhibiti wa upotevu wa mapato ulioanzishwa miezi mitano iliyopita kwa abiria au msindikizaji kulipa kiingilio kwa kutumia kadi.


Waziri amesema kabla ya matumizi ya kadi kwa siku, kituo hicho kilikuwa kikikusanya kati ya Sh 3,000,000 hadi 3,400,000 kwa siku lakini sasa wanakusanya 5,000,000 hadi 5,600,000 na kwa siku kama za matukio kama kufunga au kufungua shule inafika mpaka shilingi Mil. 6 kwa siku.


Amesema kwa yeyote mwenye kadi ambayo inatumika katika malipo mengine ataweza kuitumia na kwa ambaye hana atalipa na kupewa kadi ambayo ataitumia na kuiacha kwa ajili ya wengine.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)