Katibu Tawala wa Wilaya ya Mufindi, Bw. Frank M. Sichalwe, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kuwashirikisha wadau kwenye taftishi wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu ombi la kurekebisha bei za huduma ya maji na usafi wa mazingira kutoka kwa Mamlaka ya Maji Mafinga, leo Tar. 20/07/2023.
“niwapongeze sana EWURA, kwa hatua yao ya kuja hapa Mafinga na kukusanya maoni ya wananchi juu ya ombi hili la MAUWASA la kurekebisha bei za maji, kwani huduma hizi zinamgusa kila mwananchi na mabadiliko ya bei yanapaswa kuwa ya uwazi.
Aliongeza kwa kueleza kuwa watumiaji wa huduma ya maji wana wajibu wa kutoa maoni kwa uwazi ili kuiwezesha MAUWASA kutoa huduma bora.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Hawa Shani Lweno, ambaye ni Meneja wa EWURA Kanda ya Kati, alisema, EWURA hutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji, maamuzi yanayo tabirika na ushirikishaji wadau.
Aidha, aliwashukuru wadau na wananchi kwa mwitikio mkubwa kwenye mkutano huo.