Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi ili waweze kufanyabiashara kwa urahisi na tija.
Ameyasema hayo Julai 19, 2023 kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji(Mb.) wakati akizindua gari aina ya Ashok Leyland kutoka India chini ya Kampuni ya Usambazaji ya Kifaru Motors iliyopo nchini Tanzania katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
Aidha, Dkt. Abdallah amesema jitahada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan zinawahakikishia wafanyabiashara mazingira wezeshi na usalama wa bidhaa na watu na hivyo kuvutia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kufanya biashara nchini.