Angela Msimbira Tabora.
MICHEZO ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayoendelea mkoani Tabora kwa timu kushinda kwenye michezo mbalimbali.
Kwa upande wa mchezo wa mpira wa kikapu wavulana Unguja imeifunga Mwanza kwa pointi 25-10 wakati Mkoa wa Singida ikiichabanga Mbeya kwa pointi 19 – 18.
Pia Mkoa wa Dar es Salaam umeibuka na ushindi baada ya kuichapa Mkoa wa Songwe kwa pointi 36 -10 na timu ya Unguja iliibuka kidedea kwa kuufunga Mkoa wa Unguja kwa ponti 34-2.
Aidha kwa upande, mchezo wa tufe kwa wasichana, Denisa Conrad kutoka Kigoma ameibuka mshindi kwa kurusha tufe umbali wa mita 8.95 na kufuatiwa na Veronica Christopher kutoka Katavi alirusha tufe umbeli mita 7.57.
Kwa upande wa wavulana, ushindi umechukuliwa na Mohamed Miraji wa Manyara aliyerusha tufe umbali wa mita 8.50 na kufuatiwa na Lekunod Lemuta kutoka Arusha aliyerusha tufe umbali wa mita 8.36 na nafasi ya tatu ikishikwa na Nicolaus Chagu kutoka Songwe aliyerusha tufe mita 7.88.
Pia wanafunzi timu kutoka mikoa yote imeshindana katika mchezo wa raidha katika mbio za mita 100 kwa wasichana na wavulana na watu wenye ulemavu na mbio za mita 1,500 kwa upande wa wavulana na wasichana.