FCC kuadhimisha siku ya kupambana na bidhaa bandia duniani.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Emmanuel Kawau.

Tume ya Taifa ya Ushindani FCC June Nane Mwaka huu inatarajiwa kuungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya kupambana na bidhaa bandia.



Akizungumzia na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa FCC  William Erio amesema wataazimisha siku hiyo kwa kipindi cha wiki moja yani kuanzia June 8 hadi tarehe 15/2023 kwa kutoa Elimu kwa umma kupitia njia mbalimbali.


Ameongeza kuwa bidhaa bandia zinaathari kubwa katika soko na ushindani hivyo kuharibu biashara,kushusha thamani ya bidhaa na kufifisha uwekezaji.


"Thamani ya fedha yako haiendani na bidhaa unayoipata pia inaharibu uwekezaji" Amesema 



Katika kuadhimisha wiki hiyo FCC watatoa Elimu kwa wafanyabiashara,watoa mizigo bandarini, wanafunzi wa vyuo vikuu, pia FCC itatoa Elimu kwa umma kupitia Vyombo vya Habari mbalimbali kuhusiana na athari za bidhaa bandia ili jamii iziepuke.


Aidha kilele cha maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Dodoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Biashara na uwekezaji Dakta Ashatu Kijaji.


Kadhalika maadhimisho hayo yanaongozwa na kaulimbiu isemayo "kukuza ubia kati ya Serikali na sekta binafsi katika kupambana na bidhaa bandia".

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)