WIZARA YA KILIMO YAELEKEZWA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA ELIMU KUANZA MCHAKATO WA KUWA NA VYUO VIKUU VYA KILIMO.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na. Gideon Gregory, Dodoma.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, imeilekeza Wizara ya Kilimo kushirikiana na Wizara ya Elimu kuanza mchakato wa kuwa na Vyuo Vikuu vya Kilimo vitakavyotoa shahada zitakazoendana na mazingira.


Aidha, UVCCM imempongeza  Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwatendea haki vijana kwa kuwapa maeneo watakayoweza kuzalisha kupitia kilimo biashara.


Agizo hilo limetolewa leo Mei 24, 2023 Jijini Dodoma na Katibu wa Idara ya uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Edna Lameck wakati akitoa taarifa ya tathmini ya ziara ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mohmed Kawaida katika ziara ya ukaguzi wa mradi wa vijana (BBT).


Amesema kuanzishwa kwa vyuo hivyo kutasogeza utaalamu karibu  na wakulima na kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.


“Mnamo tarehe 17 April 2023 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana CCM ndugu Mohamedi Ally Kawaida alifanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama katika mradi wa vijana na wanawake wa Building Better Tomorrow Youth Initiatives in Agribusiness (BBT) katika vituo atamizi  9 kati ya 13 vilivyo katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Mtwara, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Kagera, Kigoma na Tabora” amesema.


Ameongeza “Mradi huu umeteua vijana 812 katika awamu hii ya kwanza ambapo vijana wa kiume ni 530 na wa kike 282, kwa sasa wizara inaendelea na dirisha la pili la vijana watakaoshiriki katika mnyororo wa thamani ikiwa ni utekelezaji wa maono ya Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Hassan Suluhu ya kuwafanya vijana wawe wazalishaji watakaotegemewa kuilisha Afrika na dunia kwa ujumla”


Edina amesema UVCCM inaona BBT ni program inayolenga kuwezesha na kuongeza Zaidi ushiriki wa vijana na wanawake katika kilimo biashara ili kuwapataia ajira, kuimarisha usalama wa chakula, kuongeza mchango wa sekta ya kilimo katika pato la taifa Pamoja na kuinua hali ya Maisha ya jamii ya watanzania.


Amefafanua kuwa kwa sasa serikali ya CCM inamawajabu ya vijana kushindwa kumiliki ardhi kwa ajili ya kilimo biashara, kukosa ujuzi masoko, mitazamo hasi na utegemezi wa kilimo cha mvua ambacho kwa muda mrefu kimeifanya sekta ya kilimo kuwa mwendo wa kobe.


“Utekelezaji wa lengo la miaka minane ya BBT la kuwa na angalau na biashara moja ya kilimo yenye faida na endelevu inayoongozwa na vijana katika vijiji 12,000 inatarajia kutengeneza ajira Zaidi ya milioni 3 ifikapo 2025/2030.


Aidha UVCCM imeelekeza Benki na taasisi nyingine za kifedha Pamoja na sekta binafsi kuunga mkono juhudi za Rais Dk.Samia kwa kushirikiana moja kwa moja na Wizara ya kilimo katika kuhakikisha vijana wa kitanzania wanapata mitaji, masoko na teknolojia za kisasa katika kushiriki kilimo biashara.


Aidha imeshauri halmshauri zote nchini zinazoshiriki katika sekta ya kilimo kutenga ardhi kwa ajili ya vijana wa BBT na vijana wote nchini na kushikiana na wizara ya kilimo kuandaa mashamba makubwa ya Pamoja ambayo tayari Dk.Samia amepeleka Zaidi ya sh.bilioni 361 kwa ajili ya miundombinu ya umwagiliaji.


“Wizara ya kilimo kuhakikisha korosho na mazao mengine hayatoki nje ya maeneo yao kwa kuyaongezea thamani na kusafirisha kutokea katika maeneo husika”.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)