Na. Gideon Gregory, Dodoma.
Wanafunzi wa chuo kikuu Cha dodoma (UDOM) wametakiwa kuachana na vitendo vya Rushwa vya kutaka kufahurishwa Katika masomo yao na wahakikishe wanakuwa mstari wa mbele kupinga na kuzuia vitendo hivyo.
Hayo yamebainishwa Rasi wa ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati Prof. Said Vuai wakati wa ufunguzi wa warsha iliyojumuisha wanafunzi wa chuo hicho pamoja na walimu Jijini Dodoma huku akiwataka walimu waachane na vitendo vya Rushwa na kuwarubuni wanafunzi kwa kuwapa msaada.
Amesema hakuna maendeleo bila ya haki na haki haiwezi kupatikana Kama Kuna Rushwa hivyo kama kijana ametumia njia ya kufauru kwa njia ya Rushwa basi hata Katika maeneo ya kazi atakayoenda kufanya yatakuwa yanachangamoto.
Kwa upande wake Mchunguzi kiongozi Takukuru mkoa wa Dodoma Faustine Malecha amesema kuwa zipo tabia ambazo zinapelekea Rushwa Moja wapo ni kuiga vitu ambavyo sio desturi ya watu wa kitanzania vinapelekea vijana kujikita Katika Rushwa huku akifafanu aina ya Rushwa na kusisitiza vijana waache kutumia Rushwa ya ngono kwa kuisi watafanikisha maisha kwa haraka.
Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kina mama na uzazi Dr. Gabriel Kitunusa amesema kuwa wanafunzi wengi wanapata Elimu zisizo rasmi huko mitaani kuhusiana na mambo ya jinsia na mambo ya uzazi na kupelekea kupata changamoto za kutoa mimba na kusababisha kifo.
Pia amesema changamoto kubwa ambao wanafunzi Hawa wanakutana nazo ni kupata mimba zisizotalajiwa na wengine kupata maambukizi ya VVU pamoja na Magonjwa ya dhinaa hivyo amewataka waachane na Elimu ya mitaani na waachane na menendo mibovu ya kimaadili.
Ikumbukwe kuwa Ndaki ya Sayansi Asilia ya Hisabati inajukumu ya kufundisha , kufanya utafiti kutoa huduma kwa jamii kupitia Katika utaaramu wa utafiti pamoja na malengo mengine yanayohusiana na Rushwa na maswala ya Afya.