RC SENYAMULE ATETA NA WADAU WA ZAO LA ZABIBU, MIKAKATI YAWEKWA KUIMARISHA ZAO HILO.

MUUNGANO   MEDIA
0

Uploading: 719309 of 719309 bytes uploaded.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule hii leo 16 Mei,2023 amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa zabibu kwa lengo la kujadili fursa na changamoto zinazokabili zao hilo ili kulipatia ufumbuzi, katika ukumbi wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma.

Katika kikao hicho kilichohusisha wakulima na wanunuzi wa zao hilo na kuhudhuriwa na Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Mhe. Deogratius  Ndejembi Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,Tawala za Mkoa na Serikali za Mtaa (TAMISEMI), Mhe. Kenneth Ernest Nollo Mbunge wa Jimbo la Bahi, Bw. Ally Gugu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Wakuu wa Wilaya tatu Chamwino, Bahi,na Dodoma Mjini kimefikia maamuzi ya kuinua zao hilo. 

Senyamule amewataka washiriki wa kikao hicho kuhakikisha wanashirikiana vizuri ili kuweza kuleta Maendeleo ya ndani ya Mkoa na taifa kwa ujumla.

“Ushirika ndio matumaini makubwa katika kutupa nguvu ya pamoja na kuweza  kukua katika kilimo, nendeni mkasimamie na kutekeleza kwa makini maazimio tuliyokubaliana kwa kuwa tukishirikiana tutafika mbali”, Amesisitiza Senyamule.

 Aidha, Mheshimiwa Senyamule amewataka wakulima wa zao hili kutumia utalaamu wa kisasa ili kuendana na mazingira ya sasa na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu, na kusisitiza matumizi ya mbolea katika kuimarisha upatikanaji wa mazao na kuongeza tija katika uzalishaji.

Senyamule pia ameipongeza Kampuni ya Jambo Food Products kwa kazi nzuri wanayofanya ya uchakataji wa zao hilo na ameahidi kuwapa eneo kwa ajili ya kuanza Ujenzi wa Kiwanda Mkoani Dodoma.

Kwa Upande Wake, Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Wizara ya Kilimo ametoa wito kwa wakulima wa zao la zabibu na wachakataji kufanya ukulima wenye tija kwa kuzingatia maelekezo ya maafisa ugani kwakuwa zao hili limeongezeka thamani kulingana na jitihada za serikali za kuwatafutia masoko ya uhakika wazalishaji na wakulima wa zao hilo.

“Serikali hatuwezi kuweka siasa kwenye Maisha ya watu lazima mikakati yetu ijibu changamoto zinazowakabili wakulima ili mwisho wa siku waweze kwenda mbele kwa kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi’’

Amefafanua Mavunde Nae, Emmanuel Ngusa Meneja Masoko wa Kampuni ya Jambo Food Product amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa ushirikiano na dhamira yake juu ya zao la zabibu na amesema lengo la kampuni mwaka huu ni kuendeleza mshikamano kwa wakulima kwa kuanza kununua zabibu kwa muda muafaka Watanunua kwa muda muafaka ambapo kwa msimu huu wanatarajia kununua tani 3000 za zabibu.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)