Ameeleza hayo wakati alijibu Swali la Mhe. Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Jimbo la Jimbo la Mbulu Vijijini, aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kumalizia ujenzi wa Vituo vya Afya Geterer na Masieda.
Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/24, Halmashauri Mbulu, imetengewa Shilingi milioni 200 kwa ajili ya ukamilishaji wa Kituo cha Afya Marekadu.
Aidha, Amesema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa Vituo vya Afya ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa Kituo cha Afya Geterer kwa kadri fedha inavyopatikana.
Ndejembi amesema Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na umaliziaji wa maboma ya Vituo vya Afya kote nchini.
