‘KUSHUKURU NI KUOMBA TENA’ NDEJEMBI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI na Mbunge wa Chamwino Mhe. Deogratius Ndejembi ameishukuru Serikali na Shirika la Kimataifa linaloratibu Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) kwa kuwezesha uboreshaji wa kituo cha Afya Dabalo kilichopo kwenye Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

Mhe. Ndejembi ameyasema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya Jengo la Upasuaji, Wodi ya Wazazi, Vifaa, Vifaa Tiba na Gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya Dabalo.

Amesema Mhe. Waziri kwa niaba ya wananchi wa Chamwino hususani ni eneo hili la Dabalo napenda kutoa shukrani zangu kwa Serikali na Wadau waliowezesha maboresho makubwa katika kituo hiki ambayo yatasaidia kutatua changamoto za kiafya ya mama na mtoto.

Hiki ndio nlichotumwa na wananchi wangu wa Dabalo na sasa kimetekelezwa hakika imani ya Wananchi hawa kwa Serikali yao na kwangu imeongezeka kupitia majengo na vifaa hivi vya Afya.

Sambamba na shukrani hizi niombe tena kwa Serikali yangu na wadau wetu kuwa bado tuna changamoto kadhaa katika kituo hiki ambazo zikitekelezwa wananchi hawa watakua wametatuliwa changamoto zao kubwa katika eneo la Afya.

Changamoto hizo ni pamoja na uchakavu wa Jengo la Wagonjwa wa Nje, kukosa chumba cha kuhifadhia maiti, wodi ya wanaume, wodi ya wagonjwa wengine, uzio pamoja na maabara.

Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) kwa ufadhili wa Serikali ya Denmark lilitoa jumla ya Sh 615,205,539 ambapo Sh 327,000,000 zimetumika kwa ukarabati na ujenzi wa kituo cha Afya Dabalo na Sh 288,205,539 zimetumika kwa ununuzi wa gari la kubebea wagonjwa na vifaa/vifaa tiba

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)