Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla ameshiriki katika maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani (May.1) yaliyofanyika katika viwanja vya Skuli ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi alikuwa Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 1 May ya kila mwaka, kwa mwaka huu yamepambwa na kauli mbiu inayosema "UWAJIBIKAJI KAZINI,MISHAHARA BORA,NA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA KAZI NDIO NGUZO MUHIMU KWA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI".
