Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa rai Kwa wadau wa Sekta za wizara yake kuzungumzia na kukemea mmomonyoko wa maadili katika jamii kwa kutumia taaluma na vipaji walivyonavyo.
"Natoa Rai kwenu Waneni (MC's) muendelee kuunga mkono juhudi za Serikali na mafanikio yake kwa kuendelea kutumia fursa zilizopo ikiwemo kupata mikopo nafuu kutoka Mfuko wa Utamaduni na Sanaa lakini pia kuwa mabalozi Wazuri wa Matumizi sahihi na sanifu ya Lugha ya Kiswahili" amesema Balozi Dkt. Pindi Chana.
Awali muanzilishi wa Chama hicho Bw. Brison Makene amesema mkutano huo una lengo la kukumbushana namna ya kuboresha kazi zao, kuzirasimisha pamoja na kubadilishana uzoefu.
Mkutano huo umewakutanisha Washereheshaji, Wahamishaji, Watunzi wa Fasihi na Wapambaji kutoka Kanda za Tanzania ikiwemo Kanda ya Kati, Magharibi, Mashariki na Kaskazini.