ZAIDI YA WATU 200 WAJITOKEZA KUPATA ELIMU YA SURUA KWA NJIA YA SINEMA MIGUNGA KATAVI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na.Elimu ya Afya kwa Umma

Elimu ya ugonjwa wa Surua pamoja na uhamasishaji wa chanjo  kwa njia ya magari ya matangazo  na sinema   imeendelea kuzaa matunda baada ya zaidi ya wananchi 200  kutoka kijiji cha Migunga kujitokeza kufuatilia kupata elimu hiyo usiku wa Machi 8.2023.

Hatua hiyo ni kutokana na Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Elimu ya Afya kwa Umma kuweka mkazo wa kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uelewa juu ya Surua na umuhimu wa kuwapeleka watoto chanjo.

Hivyo, pamekuwa na mwitikio mkubwa wa wananchi kuleta watoto wao kupatiwa chanjo baada ya kupata elimu hiyo ambapo wamekuwa wakiwaleta watoto kupata chanjo huku wakitazama sinema.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)