Fedha
hizo zitasimamiwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) pamoja na Shirika la
kuhudumia Watoto Duniani(UNICEF).
Hayo
yamejiri baada ya ujio wa ziara ya Makamu wa Rais nchini Marekani Mhe.Kamala Harris ambapo pia amesema serikali
yake kupitia Kituo cha Udhibiti wa Maradhi(CDC) inashirikiana na Tanzania katika ngazi zote ikiwemo msaada wa kitaalam katika kukabiliana na mlipuko wa Virusi vya Marburg.
Aidha,
Mhe.Kamala amesema Serikali ya Marekani itaendelea kuweka jitihada za pamoja na
serikali ya Tanzania katika utoaji wa elimu
ya afya pamoja na msaada wa vifaa tiba na
mavazi ya kujikinga (Personal Protective Equipment) katika kuwasaidia Wahudumu
wa Afya hapa nchini wanaopambana na mlipuko wa Marburg.
Kwa upande wake Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kuendelea kuwa na Ushirikiano na kubainisha kuwa nia ya Tanzania ni kuendelea kuwa na ushirikiano mwema katika nyanja mbalimbali.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni serikali ya Tanzania ilithibitisha watu watano kati ya wanane kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa virusi vya homa ya Marburg katika mkoa wa Kagera, Kaskazini Magharibi mwa nchi hii..
Hata hivyo Waziri wa
Afya , Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari Machi
21, 2023 jijini Dar es Salaam alisema Serikali imefanikiwa kuuzuia ugonjwa huo
kutoka nje ya mipaka ya mkoa wa Kagera.
Ugonjwa huo unaoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa
mwingine au kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu unatajwa kutokuwa na tiba
bali hutibiwa kwa dalili husika anazokuwa nazo mtu.