WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUSIMAMIA MAADILI YA KAZI

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na. Asila Twaha, TAMISEMI

Serikali imewataka wauguzi na wakunga kusimamia maadili na miiko ya kazi zao kwa kutoa huduma bora kwa jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe  katika Ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma wakati  akifungua kikao  cha  wauguzi na wakunga katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Ameeleza kuwa ili  mgonjwa aridhike na huduma inayotolewa kwenye vituo vya afya ni vyema kushirikiana   kuanzia ngazi ya chini mpaka juu  lengo likiwa ni kutoa huduma bora  kwa jamii.

Amewataka kuendana na mahitaji ya watu wanaowahudumia kwa   kuwa  wanapokuja kupata huduma za kiafya wanaimani kupata huduma bora.

“mbali ya kujiiona ni waajiriwa unalipwa mshahara  lakini pia tuna fungu letu kwa mungu kazi ya uuguzi na ukunga ni ibada  niwashuauri tutekeleze majukumu yetu  kwa upendo na imani” amesema Dkt. Shekalaghe.

Amewataka kuzingatia miiko na kufuata maadili ya kazi  zao kwa kuwa  itasaidia wagonjwa kuwa na  imani na huduma inayotolewa lakini watakua na imani na watoa huduma.

Ameeleza Serikali inatambua na kuthamini kazi  wanazozifanya na  pia   inajua uwepo wa   baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo Serikali itaendelea  kufanyia kazi .

Ametoa rai   kwa watendaji hao kuendelea kufanya kazi ikiwa wao ndio  wanaempokea mgonjwa kwa hatua ya awali mpaka kujua maendeleo yake.

Amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa ushirikiano   ili kuweza kutoa huduma iliyokuwa bora kwa wananchi.

“pendaneni, shirikianeni ninyi mkishirikiana mtaweza kutoa huduma iliyobora sababu itakuwa mnafanya kazi kama wamoja” 

Naye Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ustawi wa Jamii  Ofisi ya Rais, TAMISEMI Bi. Amina Mfaki akimuakilisha Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe amewataka watendaji hao kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya nchini.

Aidha, ametoa rai  kwa  viongozi wanatoka katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuendelea kusimamia  maadili ya kazi  ili kuepusha vitendo vinavyoweza kuharibu kazi na taswira ya kada hiyo.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)