Wananchi wa Kijiji cha Chiponda, Kata ya Chiponda Tarafa ya Rondo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi wamenufaika na mradi wa Uboreshaji wa Elimu Sekondari (SEQUIP) Shule ya Sekondari Chiponda Kijiji cha Tarafa ya Rondo.
Akizungumza baada ya Timu ya Watalaam
Kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Benki ya Dunia Mwananchi wa Kijiji cha Chiponda AmuriSeif Mchia walikua na njaaa ya Shule ya Sekondari lakini sasa wameshiba.
Sisi hapa tukikua na njaa ya shule na sasa tumeshiba watoto wetu walikua wanatembea Kilomita 13 kwenda shule ya Sekondari Mnarabl lakini kwa sasa wanatembea kidogo tu wamekutana na shule tunaishukuru sana Serikali na tuko tayari kwa miradi mingine.
Ujenzi wa Shule hiyo imekamilika kwa asilimia 90 na imejengwa kupitia mradi wa SEQUIP kwa gharama ya shilingi Mil. 470.
Shule ya Sekondari ya Chiponda ilo kwenye Kata ya Chiponda Tarafa ya Londo umbali wa Kilomita zaidi ya 40 kutoka Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtaman mkoani Linda.