PROF. MKENDA ZINDUA TUZO ZA WATAFITI, MSHINDI KUONDOKA NA MILIONI 50.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Machi 26, 2023 amezindua Tuzo ya watafiti wanaochapisha matokeo ya tafiti katika Majarida yenye hadhi ya juu Kimataifa Jijini Dodoma.

Katika uzinduzi huo Prof. Mkenda amesema serikali imechukua hatua iliyo amuliwa bungeni ya kutenga fedha kwenye bajeti yake kwa wale wana Sayansi na wahadhiri katika fani ya Sayansi asilia na elimu tiba ambao watafanya utafiti na kuchapisha matokeo ya utafiti wao katika majarida ya kimataifa ambapo kwa kawaida matokeo yao yatachapishwa kule kama dunia itayatambua na kuyaona kweli hapo wamesogeza sana huelewa wa binadamu katika maeneo hayo ya Sayansi na Elimu tiba.

Amesema kama wamefanikiwa kuchapisha kule waliomba bungeni wapewe fedha na kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 1 kwamba atakaye fanya hivyo atapewa Milioni 50 kama tuzo pamoja na cheti.

“Tulienda bungeni tukaomba fedha hizo zikapitishwa na ziko kwenye bajeti kwahiyo leo tumewaita ili kutangaza rasmi kuwa sasa dirisha la kupokea maombi ya wale walio weza kuchapisha matokeo ya utafiti wao katika haya majarida makubwa zaidi duniani yanayo heshimika ambayo wanasayansi wakubwa wote duniani wanapenda kuchapisha humo hivyo basi kuanzia sasa tunaanza kupokea rasmi maombi,”amesema Pof. Mkenda.

Aidha ameongeza kuwa watakao nufaika na dirisha hilo ni wale ambao machapisho yao yalitokea kati ya Julai 1,2022 hadi Mei 31,2023 ambapo tuzo hiyo itaanza kutolewa kwa machapisho katika fani ya Sayansi asilia, hisabati na tiba na huko mbeleni wataangalia uwezekano wa kuongeza machapisho katika fani ya uhandisi.

“Tumeanzia hapa tutaona tutakavyo kwenda, tuzo hii utajumuisha cheti na fedha tasrimu Milioni 50 kwa kila chapisho litakalo kidhi vigezo na kushinda, vilevile tuzo hii itatolewa kwa machapisho yote yanayo kidhi vigezo kwa mwaka husika kwa kuzingatia uwezo wa kibajeti kwa mwaka huu wa fedha wa 2022/23 serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1 kwaajili hiyo,”ameongeza.

Prof. Mkenda amesema wizara itatoa na kusambaza maelezo ya kina kuhusu muongozo na kuanza rasmi kwa mchakato kwa mwaka huu wa fedha wa 2022/23 kupitia tovuti yake ya www.moe.go.tz.

Akizungumzia vitakavyo zingatiwa amesema majarida yenye hadhi ya kimataifa yatachaguliwa kwa kuzingatia kigezo cha “IMPACT FACTOR ” hicho kikiwa ni kipimo kicho hakisi ubora wa machapisho katika majarida husika na majarida hayo.

Pia mwombaji lazima awe mtanzania kutoka taasisi yoyote ya elimu ya juu iliyopewa idhibati na mamlaka husika chini ya TCU au NACTVET.

“Tunaposema taasisi hizi haijalishi awe mtanzania tu na taasisi za elimu ya juu zenye kibali cha TCU au NACTVET bila kujali ni taasisi binafsi au taasisi ya umma, pia machapisho yatakayo shindanishwa ni yale yaliyo chapishwa katika mwaka husika kuanzia Juni 1 hadi Mai 31 ya mwaka unaofuata,”amesema.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)