SERIKALI, BENKI YA DUNIA KUSHIRIKIANA WANAWAKE KWEZESHWA KATIKA NYANJA ZOTE.

MUUNGANO   MEDIA
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amesema Serikali itahakikisha Wanawake hasa wa ngazi ya chini wanainuliwa katika nyanja zote ili kuchochea Usawa wa Kijinsia.

Dkt. Jingu amesema hayo wakati wa Kikao Kazi cha kujadili uwezeshaji  kwa Wanawake nchini kilichoratibiwa na Benki ya Dunia ,Machi 22, 2023, na kufanyika Jijini Dar es salaam.

Amesema maazimio ya Kikao kazi hicho yatasaidia Mradi wa Benki ya Dunia ambao umejikita kuchochea ushirikishwaji  na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.”Mradi wa PAMOJA”

“Ushiriki wetu kwenye kikao kazi hiki ni kiashiria tosha cha kujidhatiti kuleta Usawa wa Kijinsia nchini  na kuhakikisha kunakua na Utekelezaji wa Afua zinazowekwa ili kuwainua Wanawake kiuchumi na kuondoa ukatili wa kijinsia”Amesema Dkt jingu.

Aidha, Dkt Jingu amesema Serikali ya Tanzania inatambua kwamba Usawa wa kijinsia ni muhimili muhimu katika kuleta Maendeleo ya Taifa  na kusisitiza kuwa Usawa wa Kijinsia umebaki kuwa kipaumbele na ndiyo maana Serikali imesaini mikataba  mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuleta Usawa kwa huo.

“Kama mnavyojua Tanzania ilikua kati ya nchi zilizoshiriki  wakati wa Jukwaa la Usawa (GEF ) na Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alikubali kusimamia Eneo la pili la kuhakikisha Taifa linafikia Usawa wa Kijinsia Hivyo Wizara inaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Benki ya Dunia kuhakikasha Mradi huu unafanikiwa kwa Kufanya kazi kwa karibu na Wataalam mbalimbali kwenye Sekta zote muhimu". Amesema Jingu.

Naye, Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Nandera Mhando amesema kuna haja ya Sheria zilizopo   kuhakikisha zinamtetea Mwanamke kufanikisha masuala yanayomuhusu awapo  kazini na baada ya kustaafu.

“Licha ya ushahidi  wa maendeleo ya kiusawa wa Kijinsia tulio nao lakini bado Wanawake hawana fursa  na Haki za  Kiuchumi  kama walizo nazo  Wanaume. Usawa wa kijinsia siyo tu haki ya kibidamu bali ni Chachu ya msingi katika kuhakikisha Taifa linaendelea na kukua”Alisema Dkt Nandera.

Kwa Upande wake, Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete amesema Benki hiyo itahakikisha inafanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania ili kuhakikisha  Usawa wa kijinsia unafikiwa kama ilivyokusudiwa na Rais wa Tanzania katika Jukwaa la Usawa kwa kuhakikisha kunakuwa na uwezeshaji na ushirikishwaji wa kiuchumi kwa wanawake.

Hali kadhalika, Mtaalam wa Masuala ya Wanawake, Biashara na Sheria kutoka Benki ya Dunia, Daniela Behr amesema kuna umuhimu wa Sheria zote kuangaliwa kwa umakini kwani usawa wa kijinsia ni ngumu kufikiwa kama Sheria zilizopo katika Nchi haziwezeshi wanawake kufikia Usawa huo.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)