RAIS SAMIA AIBADILISHA MLELE KIMAENDELEO,WAFANYA KONGAMANO KUMPONGEZA.

MUUNGANO   MEDIA
0


Ni Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga akiwahutubia wananchi kueleza mafaniko ya serikali kupitia uongozi wa rais Samia ndani ya miaka miwili tangu aingie madarakani..picha na Mary Baiskeli.


Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Mpimbwe akitoa mchanganuo wa fedha zilizotolewa na rais Samia mbele ya wananchi.Picha na Mary Baiskeli.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Mlele Daniel Kifyasi akieleza mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka miwili ya uongozi wa rais Samia..Picha na Mary Baiskeli.


Mandamano yaliyoshirikisha wananchi na viongozi mbalimbali...picha na Mary Baiskeli.

  Na Mary Baiskeli, Katavi.

Serikali wilayani Mlele kupitia uongozi wa awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imepokea zaidi ya sh.196.6 bilioni kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya afya, elimu, maji, barabara na miundombinu ya umeme.

Kufuatia hali hiyo halmashauri zake za Mpimbwe na Mlele zimeungana kwa pamoja kufanya kongamano lililoanza kwa maandamano ya amani lengo ni kumpongeza rais kwa utendaji kazi wake uliotukuka.

Kongamano hilo limefanyika viwanja vya shule ya msingi Majimoto March 21,2023 huku wananchi wakipata ufafanuzi wa matumizi ya fedha hizo zilizotolewa na serikali na uhalisia wake.

Mkuu wa wilaya ya Mlele Majid Mwanga akiwahutubia wananchi kwenye kongamano hilo amesema jitihada zinazofanywa na Mhe.rais za kuboresha miundombinu mbalimbali hazina kifani.

“Ndugu zangu Wanamajimoto nafahamu mnaathirika sana na umeme wa kukatikatika lakini rais wetu ameshatenga zaidi ya sh52 bilioni za kujenga miundombinu ya umeme kuja hadi Mpimbwe,”

“Wale mnaosafiri na barabara ya kwenda Tabora mmeona nguzo nyingi zimewekwa, hayo ndo matamanio ya rais ya kuachana na umeme wa jenereta na mafuta tuingie kwenye gridi ya taifa,”

Amesema umeme huo utakapofika Mpimbwe utasaidia viwanda vinavyofanya kazi kwa kutojiamini vitaweza kuzalisha zaidi.

SEKTA YA MAJI.

Katika wilaya ya Mlele awali kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji lakini ndani ya miaka miwili ya uongozi wa rais Samia imekuwa historia katika maeneo yao.

“Sekta hii ya maji pekee Mhe.rais ameleta zaidi ya sh.26 bilioni siyo pesa ndogo ndiyo maana mnaona miradi kemkem katika halmashauri ya Mpimbwe na Mlele,”

“Niwaombe sana tuilinde, kuithamini na kuithamini miundombinu ya RUWASA na tuendelee kumuombea rais wetu ili kutujali Wanamlele,”

MIUNDOMBINU YA BARABARA.

Ili kuondokana na tatizo la ubovu wa barabara linalowarudisha nyumba wafanyabiashara kusafirisha mazao na bidhaa zingine rais Samia ametoa sh.88 bilioni zinazojenga barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa zaidi ya 50 kutoka Kibaoni hadi Stalike.

Sanjari na hayo amelipondeza kundi la waganga wa tiba asilia kushirikiana na watoa huduma za afya kufanikisha utolewaji chanjo ya surua kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

“Lengo lilikuwa kuchanja watoto thelathini na tisa elfu katika halmashauri ya Mpimbwe kutokana na kata ya Majimoto kuathirika zaidi na surua,”

“Nafurahi kuwaeleza kuwa zaidi ya watoto arobaini na nne elfu wamepata chanjo hiyo katika halmashauri ya Mpimbwe,”

Mafanikio hayo yamepatikana baada ya serikali ya wilaya kuwaomba waganga wa jadi wawatibu wagonjwa wao baada ya kumalizana nao wawapelekee watoa huduma za afya.

Mbali na hayo ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na serikali kupinga vitendo vya rushwa huku akiwaahidi wafugaji kutatua changamoto zao haraka iwezekanavyo.

“Tutakaa nao tutazungumza nao lakini nao watambue wajibu wao wasiingize ng’ombe ndani ya hifadhi ya Katavi,mwisho tuendelee kumshukru rais kwa yale anayotutendea Watanzania,”amesema.

MCHANGANUO WA FEDHA HIZO HALMASHAURI YA MPIMBWE NA MLELE.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mpimbwe Catherine Mashala amesema katika kipindi cha miaka miwili kupitia serikali ya awamu ya sita imewezesha kupokea zaidi ya sh.10 bilioni.

“Fedha hizi zimetekeleza miradi ya maendeleo na shughuli za wananchi,sekta ya afya tumepokea shilingi bilioni nne na milioni mia sita arobaini na moja,”

“Zimejenga majengo tisa kwenye hospitali yetu ya wilaya, vituo vya afya vitatu kikiwemo kilichotumia mapato ya halmashauri cha Majimoto,”

Amesema fedha zingine zimejenga zahanati 5,kununua vifaa tiba, yamefanyika maboresho ya huduma ambapo hospitali yao ya Mpimbwe ina kitengo cha meno ambacho kina vifaa vyote.

SEKTA YA ELIMU MPIMBWE.

Kwaupande wa sekta hiyo fedha zilizopokelewa ni zaidi ya sh.3 bilioni zimetumika kujenga madarasa 102 yakiwamo ya Uviko 19 na kapu la mama limejenga madarasa 72.

“Tumejenga matundu ya vyoo tisini,ununuzi wa thamani madawati shule za msingi, viti na meza kwa shule za sekondari,”

UWEZESHAJI VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU.

Makundi haya yamewezeshwa kupata mikopo ya sh.393 milioni zilizotolewa kupitia mapato ya asilimia 10 ndani ya miaka miwili.

Vikundi hivyo vimewezeshwa mashine za kuchakata alizeti,unga, mchele na mashine za kufyatua tofali lakini tuna kitendo cha B.fedha na biashara kimekusanya zaidi ya sh.3 bilioni.

SEKTA YA MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA.

Halmashauri imepokea sh.153 milioni kutoka serikalini ambazo zimetumika kuanzisha kitalu cha miche kila kata imepatiwa miti kwaajili ya kupanda.

“Nawaomba wananchi tutoe ushirikiano kwaajili ya kurejesha uoto wa asili,Idara ya ardhi imepokea sh.627 ambazo zimetumika katika sensa na anwani za watu na makazi,”

SEKTA YA KILIMO,MIFUGO NA KILIMO.

Sekta hii ndani ya miaka miwili imepokea sh.91 milioni,zimetumika kuboresha skimu ya Kilida kwa gharama ya sh.61 milioni itasaidia wakulima kuzalisha mazao misimu yote.

“Tulikuwa na eneo la ukarabati wa machinjio hapa Majimoto bado tupo kwenye hatua za maboresho ili tupate nyama yenye ubora,”

“Kama halmashauri tulipokea tani 87 za mbolea ya ruzuku ambayo ilisambazwa maeneo yote ya wakulima wa Mpimbwe,wito wangu tuzalishe kwa wingi kwasababu kwasasa soko siyo tatizo,”

MAMBO MENGINE YALIYOTEKELEZWA NA SERIKALI.

Ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara ya Majimoto na Senkwa ikiwamo utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji kutoka Majimoto kwenda Usevya, barabara ya Kibaoni kwenda Inyonga ipo kwenye ratiba ya matengenezo.

“Mambo yote haya yamefanyika katika kipindi cha awamu ya sita inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan, naomba niungane na Watanzania wote kuipongeza serikali kwa hatua hii,”.

HALMASHAURI YA MLELE

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mlele Daniel Kifyasi amesema fedha walizopokea kutoka serikalini kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ni zaidi ya sh.1 bilioni.

SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO.

Amesema sekta hiyo ni mama kwa wananchi wa halmashauri ya Mlele kwakuwa wengi wanaitegemea kuongeza mapato kupitia uzalishaji hivyo wamepokea zaidi ya sh.800 milioni.

“Tumepokea pikipiki 12 na tani 343 za mbolea ya ruzuku yenye thamani ya zaidi ya sh.480 milioni,Elimu sekondari tumepokea zaidi ya sh.1 bilioni zimetekeleza ujenzi wa vyumba vya madarasa,”

“Uboreshaji wa miundombinu na ukarabati wa madawati, barabara ya kutoka Tabora kwenda Mpanda baada ya kujengwa kwa kiwango cha lami imekuwa chachu kwa uwekezaji,

“Jumla ya viwanda vidovidogo 915 vimejengwa na vinatoa ajira kwa zaidi ya watu 400, tunao pia mkakati wa lishe ambapo kila mtoto ametengewa sh1000 ikiwa ni takwa la kisheria,”

Hata amemuomba Mkuu wa wilaya hiyo kufikisha salaamu kwa rais kuwa wanatambua kazi anayofanya na wanaendelea kumuunga mkono.

Mmoja wa wakazi wa Majimoto Anjeli Edward Mwakalinga amesema wanamshukru rais kwa juhudi anazofanya kwakuwa ameboresha huduma za jamii tofauti na ilivyokuwa awali.

“Ni muda mfupi tangu aingie madarakani ameboresha shule,barabara, afya, maji na mengine hatuna tatizo naye aendelee kufanya kazi tunampenda sana,”

Wilaya ya Mlele ni moja ya wilaya zilizopo mkoani Katavi ambayo inakuwa kwa kasi kutokana na uwepo wa fursa za kiuchumi na miundombinu ya huduma za kijamii imeboreshwa ipaswavyo

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)