MNAWAJUA MLIO WAKOPESHA WAAMBIENI WARUDISHE MIKOPO - KAMATI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na. Asila Twaha, Nachingwea.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imeutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kuwafuatilia wale wote waliopewa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri kurejesha mikopo hiyo kutokana na Kanuni na Mikataba waliyokubalina kwa sababu wanawajua waliowakopesha. 

Hayo yamesemwa tarehe 21 Machi, 2023 na Kamati hiyo ilipokutana na Watendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Nachingwea ikiwa kamati hiyo nimuendelezo wa ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi katika Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mhe. Halima Mdee (Mb) akiambatana na wajumbe wa kamati hiyo walioonesha kutokuridhishwa kwa kukinzana kwa taarifa iliyosomwa na mwakilishi wa Ofisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Kamati hiyo kuutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Nachingwea kujiridhisha na maelezo yao kwa sababu Kamati imesema lengo lao ni kuona utekelezaji wa matumizi na usimamizi wa fedha za Umma vinasimamiwa kwa nidhamu.

“Kama kuna eneo kamati italivalia njuga ni hili mikopo ya asilimia 10 mnayokopesha tunataka mkikopesha irudi iwasaidie na wengine" 

Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Mhandisi Chionda Kawawa alisoma taarifa yake ambayo ilikinzana na taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Lindi jambo lililoibua sintofahamu kwa Kamati hiyo.

Nitoe rai ninyi Watendaji ambao mmeaminiwa mtekeleze wajibu wenu, haitakubalika sisi tulioaminiwa kufuatilia matumizi ya fedha za Umma halafu ninyi ambao ni Watendaji msitekeleze wajibu wenu” Mhe. Halima Mdee.

 Amewataka Watendaji katika eneo la mikopo wajipange sababu eneo la mikopo ya asilimia 10 litasimamiwa na Kamati hiyo kikamilifu na kuwataka kuweka vizuri taarifa zao ili iendane na taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali sababu jicho la Kamati hiyo ni taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

“haiwezekani mkopeshe vikundi halafu pesa hizo zisirudi hatukuja kufunika kombe mwanaharamu apite kamati imetumwa kutekeleza majukumu yake kama ambavyo imeaminiwa kufanya kazi na itafanya kazi” amesisitiza Mhe. Mdee.

Amefafanua fedha za mikopo ya asilimia 10 zikisimamiwa vizuri na ninyi watendaji mliopewa na kuamniwa kuzisimamia zitawasadia watu wengi kuweza kujiajiri kutokana na changamoto za ajira zilizopo na pia mkiisimamia vizuri tunategemea itapunguza utegemezi na watu kuweza kujiajiri na hata kupata wawekezaji katika nchi yetu.

Kamati imetoa ushauri kwa Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kuiweka sawa taarifa yao lakini pia kuona ni jinsi gani fedha hizo zilizokopeshwa zinarejeshwa kutokana na mikataba waliokubaliana na vikundi mbalimbali.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)