Kamati ya Kudumu ya Bunge hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe, Halima Mdee imepokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhusu Utawala na Uendeshaji wa Serikali za Mitaa nchini.
Kamati hiyo pia imepokea taarifa ya Vyanzo vya mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa, na Utaratibu wa upatikanaji wa ruzuku ya Serikali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 14 Machi 2023 Bungeni jijini Dodoma na kuhudhuliwa Wakuu wa Idara na watoa taarifa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI wakiongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange.
Kamati za Kudumu za Bunge zinaendelea na vikao vilivyoanza tarehe 10 Machi 2023 na vinatarajiwa kumalizika tarehe 31 Machi 2023 kabla ya kuanza kwa Mikutano ya Bunge.
