KATAVI BADO INAKABILIWA NA UGONJWA WA MALARIA KIWANGO CHA JUU IKILINGANISHWA NA KILE CHA KITAIFA

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na Mary Baiskeli, Katavi.

Licha ya ugonjwa wa malaria kupungua nchini Mkoa Mkoa wa Katavi bado unakabiliwa na tatizo hilo ambapo kati ya watu 100 waliopimwa katika Kijiji cha Vikonge wilayani Tanganyika 29 wamekutwa na maambukizi tofauti na idadi ya wanane wa mikoa mingine.

Wakazi wa kijiji cha Vikonge wilaya ya Tanganyika juzi wakiwa katika katika uzinduzi wa kampeni ya ”SHINDA MALARIA”iliyofadhiliwa na Shirika la maendeleo la Marekani USD na kuratibiwa na Taasisi ya utafiti wa malaria Ifakara wametaja sababu zinazopelekea tatizo hilo kuwa ni umbali wa kutolea huduma za afya.

Martine Mawemeza mkazi wa Kijiji cha Vikonge alisema kabla ya kampeni hiyo walipata adha kubwa ya upatikanaji wa huduma za afya inawaliwalazimu kutumia gharama kubwa ya nauli kwenda Mpandadogo umbali wa zaidi ya kilometa 40.

“Gharama ya usafiri ni aidi ya sh30,000 wengi wanashindwa kumudu kutokana hali duni ya maisha hivyo wanapoteza watoto wao kwa ugonjwa wa malaria,

“Hii huduma ya nyumba kwa nyumba kupitia kampeni ya shinda malaria itasaidia kupunza vifo kwa watoto wetu tunamshukru sana rais,”alisema Mawemeza.

Elizabeth Emmanuel alisema vifo vingi vya watoto vinatokea kutokana na kushindwa kufikishwa kwenye huduma kwa wakati na hiyo inasababishwa umbali na miundombinu mibovu ya barabara.

“Vituo vya afya vipo mbali sana ukilinganisha jiografia yetu siyo rafiki, usafiri wa shida na watu wengi tunaishi pembezoni mkoa umezungukwa na mistu ilituathiri lakini kwasasa tutapata ahueni,”alisema Elizabeth.

Mtendaji Mkuu wa mradi wa shinda malaria kutoka Taasisi ya afya Ifakara Daktari Dunstan Bishanga alisema kabla ya uzinduzi huo walifika Kijiji cha Luhafwe na kubaini hakuna kituo cha afya.

“Wananchi wanalazimika kuja Vikonge kupata huduma umbali wa kilometa 39 na Mwenyekiti wa Kijiji ametuambia ana watu zaidi ya 30,000 wote wanategemea kutibiwa hospitali ya Majalila,”

“Niliuliza swali ikitokea mtu au mtoto akiugua wanafanyaje?wakadai inabidi kutafuta pikipiki kwa gharama ya sh30,000 hadi hospitali ndiyo maana tunapigania wawepo watoa huduma ngazi ya jamii,”alisema Bishanga.

Mwakilishi wa shirika la maendeleo la Marekani USD Lulu Msangi alisema mpango wa kupambana na malaria katika mkoa wa Katavi wametoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika vijiji 36 vya halmashauri ya Tanganyika na Nsimbo.

“Tumetoa vyandarua mashuleni na vituo vya afya, baiskeli 2, mikoba ya kuweka vifaa, vipima joto 2, mizani ya kupima uzito ya wagonjwa, simu za mkononi na vinginevyo vyenye thamani ya sh47.5milioni,”

Naye Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu alisema pamoja na jitihada hizo ni vyema wadau hao watafute mbinu mbadala za kuua mazalia ya mbu.

“Tunafahamu wilaya yetu ina mapori mengi yanayosababisha mbu kuzaliana kwa kasi tafuteni mwarobaini wa kudhibiti mazalia ya mbu,”alisema Buswelu.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko mgeni rasmi katika uzinduzi huo aliwataka Wakurugenzi wa halmashauri kuwasimamia kikamilifu waganga wakuu na watumishi waliopewa dhamana katika mradi huo.

“Kama adhma ya mradi ilivyoelezwa itahudumia wananchi walio umbali mrefu kutoka kwenye huduma za kutolea huduma za afya asiwepo mtumishi wa kukwamisha,”alisema Mrindoko.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)