KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA MUUNDO WA MAMLAKA YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA (DCEA).

MUUNGANO   MEDIA
0

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza  wakati wa semina ya kuwajengea uwezo  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Ukumbi wa Bunge Machi 20, 2023 Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akifafanua jambo wakati wa semina hiyo.


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria  wakifuatilia semina iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kuhusu muundo wa Mamlaka hiyo na majukumu yake katika  Ukumbi wa Bunge Machi 20, 2023 Jijini Dodoma.

Kamishna  wa Sheria kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bi Veronica Matikila  akitoa wasilisho kuhusu sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Namba 5 ya mwaka 2015 mbele  ya  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika  Ukumbi wa Bunge Machi 20, 2023 Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea na kujadili muundo wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) nchini.

Kikao hicho kilichofanyika Machi 20, 2023 Jijini Dodoma kimeongozwa na  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph  Mhagama  na kuhudhuriwa na wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na wadau mbalimbali.


Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)