AJALI YAUA 9 KATAVI

0

 


Na.Mary Baiskel,

Katavi.

Watu 9 wamepoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa bàada ya basi la kampuni ya Kombas lenye namba za usajili T 506 walilopanda wakati likitokea Kigoma kuja Mpanda kuacha njia na kupinduka kwenye korongo la mlima Nkondwe wilayani Tanganyika.

 Ajali hiyo imetokea Machi 06 saa 9:45 mchana ambapo imeelezwa kuwa baada ya kufika eneo la mlima Nkondwe basi Hilo liliserereka hadi kwenye korongo hilo lenye kina cha mita zisizopungua 75 chini yake kukiwa na mto.


Mganga Mkuu hospitali ya wilaya ya Tanganyika ...Mrema amesema vifo hivyo vimetokea papo hapo ambapo wanaume walikuwa  watano Kati yao watoto mtoto mmoja anakadiriwa kuwa na umri (2) na watatu na watu wazima wawili.


"Wanawake wanne pia wamepoteza maisha wote watu wazima Kati ya umri (18-22)na mmoja   umri 30-35,mwingine alikuwa mjamzito,"amesema Mrema.


Aidha amesema Kati ya  majeruhi 30 baadhi yao wamepokelewa hospitalini hapo na wengine wanne wamepelekwa hospitali ya rufaa mkoa wa Katavi huku wengine wakitibiwa na kuondoka.

 

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo Raphael Lutonja amesema alipigiwa simu Kisha kupewa taarifa hizo na baada ya kufika eneo walikuta abiria wamekandamizwa wakaanza kuwanusuru.


"Baadhi yao walikuwa wamepoteza maisha,tunaomba serikali itusaidie hili eneo kwasababu ajali zinatokea mara kwa Mara,"


Mmoja wa Majeruhi wa ajali hiyo Philberth Bugeraha aliyelazwa hospitali ya wilaya ya Tanganyika amesema walipokaribia kwenye Kona hiyo gari lilikwenda kwa mwendo Kasi mithili ya breki kufeli.


"Kona ikishindikana ikapitiliza hadi shimoni,baadaye niliona kama giza nikafumbua macho nikaona nimeumia mkono nimo ndani gari lemeinama nikajikwamua kutoka,"amesema Bugeraha.


Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba wanaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.


"Lakini tunatoa nasaha kwa madereva wetu kuwa makini na kchukua tafadhari kubwa Sana waapopita kwenye milima hatarishi kama huu wa Nkondwe ni hatari mkoani kwetu,"amesema Makame.Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amefika hospitali ya wilaya ya Tanganyika kutoa pole kwa wahanga. "Nawapa pole wafiwa na majeruhi huduma zinaendelea kutolewa na utambuzi wa maiti utatolewa baadaye kupitia vyombo vya habari" amesema Mrindoko.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)