WAZIRI CHANA AIKARIBISHA UAE NA WAWEKEZAJI WENGINE KUWEKEZA KWENYE HEWA YA UKAA

MUUNGANO   MEDIA
0

 


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana ameikaribisha Kampuni ya Blue Carbon ya UAE na wawekezaji wengine kufanya biashara ya hewa ukaa na Serikali ya Tanzania.

Waziri Balozi Dkt. Chana ameyasema hayo leo Jijini Dodoma  mara baada ya Taasisi ya Blue Carbon UAE na Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutiliana saini mkataba wa makubaliano

Mkataba huo umelenga kuanzisha  ushirikiano wenye lengo la kukuza usimamizi endelevu wa misitu, kukabiliana na ukame na kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi.

Amesema kwa miaka mingi, changamoto za usimamizi wa misitu ni ukosefu wa motisha kwa jamii na serikali ya kulinda msitu.

“Miradi kutoka kwa mipango ya mikopo itatoa motisha ya moja kwa moja na kukuza ulinzi wa misitu na usimamizi endelevu. 

Ni matumaini yetu kwamba yaliyomo katika mkataba wa makubaliano yatachangia juhudi za taifa.”

Waziri Dkt. Chana ameishukuru serikali ya UAE kuingia mkataba huo ambao umefungua milango katika sekta hiyo muhimu na kusisitiza kuwa serikali imeipa kipaumbele katika upande wa hewa ukaa.

“Hewa ukaa ni eneo jipya na wakati umefika sasa wizara yangu na wizara ya mazingia kuangalia namna ya kuimarishwa hili. Rai yangu kwa wananchi ni kuwa tuna misitu vya vijiji, halmashauri, ya watu binafasi ya hifadhi basi tuitunze na tuilinde maana tunapata mazao mapya ya misitu.”

Kwa upande wa Mwanamfalme na Mwenyekiti wa Taasisi ya Blue Carbon, Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum amesema “ Ni heshima kubwa kusaini Mkataba huu na Serikali ya Tanzania. Ushirikiano huu unawakilisha hatua muhimu katika kukuza mazoea ya usimamizi endelevu wa misitu na kupambana na mabadiliko ya tabianchi"

Naye Kamishna wa Uhifadhi TFS, Prof. Dos Santos Silayo alisema wakati umefika sasa kwa nchi zilizoendelea kuweka mchango wao kwa nchi zinazoendelea kupunguza gesi joto.

Amesema hatua ya kusaini makubaliano na Blue Carobon ni mwanzo wa utekelzaji wa shughuli hizi na kuwa kampuni hiyo itaanza mchakato wa kusajili kwa kuzingatia sheria zinazozingatia  biashara ya hewa ukaa ya mwaka 2022.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)