WAZIRI BALOZI DKT.CHANA : TUMEDHAMIRIA KUPUNGUZA MIGONGANO KATI YA BINADAMU NA WANYAMAPORI

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha migongano kati ya binadamu na wanyamapori inapungua kwa kiasi kikubwa.

Ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam wakati akiwaeleza Wabunge wa Bunge la Ujerumani waliokuja Tanzania kwa lengo la  kukagua na kujionea miradi mbalimbali ya Uhifadhi  mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Ujerumani.

'' Hatuwezi kuzungumza shughuli za uhifadhi pasipo kuitaja Serikali ya Ujerumani kwani ni wadau muhimu wa Uhifadhi ,Tumekuwa tukishirikiana kabla na baada ya nchi yetu kupata uhuru" amesema Balozi.

Akitaja jitihada hizo, Balozi Chana, amesema Serikali imechukua uamuzi wa kujenga vituo vya kudhibiti wanyamapori hao  kabla  hawajaleta madhara kwa binadamu  pamoja na mali zao.

Ameongeza kuwa Serikali imeanza kutumia mfumo wa kigitali wa kuangalia mienendo ya makundi ya tembo kabla hajafika katika makazi ya wananchi na kwenye mashamba yao kwa kuwawekea vifaa maalum.

Amefafanua kuwa mfumo huo umeweza kufanyika katika Hifadhi mvalimbali ikiwemo Ruaha, Mikumi na Serengeti na kumekuwa na matokeo chanya ya kuwadhibiti wanyama hao.

Aidha, Balozi Chana amewaeleza Wabunge hao kuwa Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa wananchi wanaoishi kando kando mwa Hifadhi namna ya kujihami na kuwadhibiti wanyaapori hao pindi wanapokaribia katika makazi yao na hilo limeweza kuleta mafanikio.

Amebainisha kuwa kabla ya mafunzo hayo katika maeneo mengi nchini watu wengi walijeruhiwa na wengine waliuawa kutoka na kukosa maarifa ya namna ya kujihami ambapo amesema watu wengine walikuwa wakiwafukuza kwa fimbo na wengine kudiriki kupiga na tembo.

Kufuatia hali hiyo, Balozi Chana ametoa wito kwa Wabunge hao kuwa shughuli za uhifadhi nchini zinahitaji fedha ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo ya muingiliano wa wanyamapori.

Kwa upande wake Ujumbe kutoka Ujerumani ukiongozwa Knut Gerschau ameipongeza Tanzania kwa kazi kubwa ya shughuli za uhifadhi inazofanya na kuahidi kuwa ushirikiano huo katika nyanja za uhifadhi ni muendelezo wa shughuli za uhifadhi.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)