TBA YAENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM YA UTENGENEZAJI WA MAKAZI BORA KWA WATUMISHI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na Gideon Gregory, Dodoma.

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) amefanikiwa kuendelea kutekeleza Malengo Waliyojiwekea kwenye mpango mkakati wa mwaka 2021/22 hadi 2025/206 pamoja na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 inayowaelekeza kusimamia na kuhakikisha utengenezaji wa makazi bora kwa watumishi.

Hayo yametanabaishwa leo Februari 14,2023Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Mtendaji wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Daudi Kondoro mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea utekelezaji wa majukumu wa wakala huyo katika kipindi cha miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia.

Amesema wameendelea kutoa huduma ya uhakika ya makazi kwa serikali na kwa watumishi wa umma kwa kutoa huduma ya uhakika ya makazi ya nyumba ambapo mpaka sasa kuna nyumba 1,622 zimepangishwa kwa watumishi wa umma na pamoja na nyumba 7,700 zimeuzwa kwa watumishi wa umma Tanzania bara.

“Katika ilani ya chama cha Mapinduzi kuna maelekezo mahususi kwa wakala wa Majengo Tanzania ibara ya 55 sehemu H kuanzia kipengele cha kwanza hadi cha nne kinataka wakala wa Majengo uweze kusimamia na kuhakikisha kwamba inatengeneza makazi bora lakini pia baadhi ya maeneo ambayo yamerejeshwa.”amesema Kondoro.

Aidha ameongeza kuwa TBA imetengeneza fursa za ajira na kutoa mafunzo kwa vitendo ambapo imetengeneza ajira takribani 100,000 kwa vijana walio na ujuzi na ambao hawana ujuzi kupitia miradi ambayo imekua ikitekelezwa.

“Naishukuru sana serikali ya Rais Dk. Samia kwa kuendelea kuiwezesha TBA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali. katika kipindi cha miezi 18, tayari imetoa sh. bilioni 54.2 ajili ya utekelezaji wa miradi,”amesema.

Sambamba na hayo Kondoro amesema miradi iliyotekelezwa katika kipindi husika kuwa ni mradi wa ujenzi wa nyumba 3500 za watumishi wa umma katika eneo la Nzuguni Dodoma ambapo mradi huo uliwekwa jiwe la msingi na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango Novemba 30 mwaka jana.

“Serikali imeshatoa sh.bilioni 15.5 kwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 150 ambao umefikia asilimia 81 na awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba 150 za awamu ya pili ukiwa umefikia asilimia tatu,”amesema Kondoro.

Pia, ametaja mradi mwingine kuwa ni ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma katika eneo la magomeni kota, awamu ya kwanza na ya pili ambao unagharimu sh.bilioni 7.8 na ujenzi wa jengo la ghorofa nane lenye uwezo wa kuchukua familia 16 tayari limeshakamilika kwa asilimia 99.

“Mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi jijini Dodoma ambao umegharimu sh.bilioni tisa mradi huu ulitekelezwa ili kukabiliana na uhaba wa nyumba za makazi ya viongozi uliojitokeza mara baada ya serikali kuhamishia makao yake makuu jijini Dodoma mradi huu umeshakamilika kwa asilimia 100,”amesema.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)