Na Emmanuel Kawau.
Mkuu wa wilaya Temeke Mwanahamisi Mkunda Amewataka vijana wenye taaluma mbalimbali kuunda vikundi na kuanda wazo la biashara na kuomba mkopo wa halmashauri usio na Riba na kutengeneza ajira mpaya kwenye jamii na kuacha tabia ya kulalamika kila mara kuwa hamna ajila.
Hayo ameyasema katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya ujasiliamali, usimamizi wa biashara na fedha kwa vikundi 183 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wanaonufaika na 10% ya mapato ya ndani 2022/2023 katika wilaya Temeke, Dar es salaam na kuwasisitiza wanufaika kurejesha fedha kwa wakati ili wengine waweze kunufaika.
Mwanahamisi amebainisha kuwa mfumo wa utoaji mikopo ngazi ya halmashauri unatatua changamoto zaidi ya moja kwenye jamii, na Mh rais samia anataka kila mwananchi awe na uchumi imara,anataka taifa lenye uchumi jumuishi piaTokea kuanza kwa utoaji mikopo hiyo kumechochea kuzalisha ajira mpya nyingi kwenye jamii za watu wamaisha ya kawaida.
Kwa upande wake Afisa biashara manispaa ya temeke judith matage Amewakumbusha wajasiliamali na wafanyabiashara kukata leseni za biashara na kwamba ni takwa la kisheria kabla ya kufungua biashara unatakiwa ukate leseni kwanza na ni lazima uzininginize ukutani.
"Ukiomba leseni ni masaa 24 tu,vikundi vyote mnatakiwa muwe na leseni,mahitaji yake ni lazima muwe na katiba,muhtsari,TIN,Mkataba wa pango,cheti cha usajili wa vikundi cha mwisho ni vitambulisho vyenu,vingine ni vya kibiashara niwakaribishe ofisini" Alisema Judith.
Afisa vijana Manispaa ya Temeke Anna marika amebainisha fursa za biashara katika makundi yote matatu,kama mnabiashara zinaweza kununuliwa na serikali ambazo ni watoa huduma mbalimbali kwa mfano biashara ya chakula,uzalishaji wa bidha au vifaa,ujenzi, ni lazima kikundi kiwe kimsajiliwa,kuwe na account ya Bank,
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Temeke Abdalah Mtinika amesema mpaka sasa takribani bilion 11.87 zimetolewa pia amesema hapo awali marejesho ya mkopo yalikuwa yakisuasua na kuwa asilimia 20% pekee kwa sasa hamasa imeongezeka na kufikia 60% ya marejesho.
Akitoa ushuhuda moja ya kikundi kilichonufaika na mikopo cha Taifa kwanza Mwakilishi wao Christopha Mjema amesema waliomba Mkopo mwaka 2019 mwaka 2020 walipewa kiasi cha fedha cha milioni 40 wakaanzisha kampuni ya uuzaji pikipiki na wamefanikiwa kuajiri vijana 9 na mpaka sasa wamekuza mtaji na kufikia milioni 68 na mwezi wa saba mwaka huu wanatarajia kukamilisha marejesho ya mkopo huo.