WAMILIKI WA MAGARI WATAKIWA KUHAKIKISHA MAGARI YAO YANAKAGULIWA
Jumatatu, Februari 06, 2023
0
Na Emmanuel Kawau.
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limezindua kampeni ya ukaguzi wa usalama wa vyombo vya moto nchi nzima na kugawa stika maalumu kwa gari zilizokaguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 6, 2023, Mkuu wa Kikosi cha Usalam Barabarani Ramadhani Ng’anzi amesema kampeni hiyo itahitimishwa Machi 13 mwaka huu.
kamanda king'azi ametumia fursa hiyo kuwaagiza Wakuu wa Vikozi vya Usalama Barabarani Mikoa (RTO) kutenga maeneo ya ukaguzi huo kuanzia leo na kuwataka madereva na wamiliki wa vyombo vya moto kuonyesha ushirikiano.
“Lengo la ukaguzi huu ni kuhakikisha kunakuwepo na usalama wa vyombo vya moto ili kupunguza ajali za Barabarani. Kampeni hii itahitimishwa Machi 13 mwaka huu Wiki ya Usalama Barabarani,” amesema Kamanda Ng’anzi.
Ameongeza kuwa vyombo vyote vitakavyofanyiwa ukaguzi vitapatiwa stika maalumu na baada ya kipindi cha ukaguzi kuisha chombo chochote kitakachokuwa hakijakaguliwa na endapo kitakutwa na shida kitaondolewa barabarani mojo kwa moja.
Kadhalika amebainisha mchango wa gharama za ukaguzi huo kuwa,kwa magari ya biashara ni TZS 7,000, magari binafsi ni TZS 5,000, Bajaji na Pikipiki TZS 2,000.

