SERIKALI YAFUNGUA MILANGO YA USHIRIKIANO WA BIASHARA NA MAREKANI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Serikali imesema imefungua milango ya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Marekani kupitia Sekta Binafsi ili kuchochea biashara na uwekezaji ikiwa ni utekelezaji wa mazungumzo kati ya Marais wa nchi hizo mbili yaliyofanyika hivi karibuni mjini Washington DC.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba walipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Biashara wa Marekani, Bi. Marisa Lago Februari 07, 2023 jijini Dodoma.

Dkt. Kijaji amewaalika tena wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Marekani kuendelea kukaa na kufanya mazungumzo na Serikali  kwa kuwa Serikali ipo tayari kuhakikisha kuna wekezaji wa kutosha na wenye tija.

Aidha, Dkt. Kijaji alieleza kuwa kuna jumla ya miradi 271 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 4.8 inayomilikiwa na wawekezaji kutoka Marekani ikiwemo miradi 68 ya Maliasili na Utalii na miradi miradi 66 ya kilimo inayoongeza thamani ya mazao na hivyo kuongeza ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Aidha Dkt. Kijaji amewaalika tena wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Marekani kuendelea kukaa na kufanya mazungumzo na Serikali  kwa kuwa Serikali ipo tayari kuhakikisha kuna wekezaji wa kutosha na wenye tija.

Naye Dkt. Nchemba amesema kuwa Tanzania ina maeneo mengi yenye fursa za uwekezaji ikiwa ni pamoja na viwanda, kilimo, madini, uchakataji ngozi, nyama, madini lakini pia vifaa tiba, utalii, uchumi wa blue na mengine.

Aidha Dkt. Nchemba alimwahidi Naibu Waziri huyo kuwa Serikali inaendelea kuboresha mifumo ya ukadiriaji na ukusanyaji kodi kwa njia ya kidigitali ili kutenda haki, kuweka taratibu bora za ununuzi ili kukuza biashara na uwekezaji hapa nchini.

Naye Naibu Waziri wa Marekani anayeshughulikia masuala ya biashara, Bi. Marisa Lago aliihakikishia Tanzania kuwa Marekani iko tayari kuimarisha zaidi masuala ya biashara na uwekezaji kupitia sekta binafsi kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni hatua ya kuunga mkono dhamira ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukuza uchumi wa nchi kwa faida ya watu wake.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)