KIKAO CHA KUANDAA MPANGO KAZI ELIMU YA AFYA KWA UMMA 2023/2024 KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU CHAANZA RASMI ARUSHA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na.Elimu ya Afya Kwa Umma-Arusha.

Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma (HPS) imeanza kikao kazi cha pamoja kati ya Wadau wa Maendeleo na Serikali kuhusu kuainisha vipaumbele na mikakati ya utekelezaji (Health Promotion priority interventional activities) kwa mwaka 2023/2024.

Kikao kazi hiki kinalenga kuwa na Mpango wa Utekelezaji wa Afua za Elimu ya Afya kwa Umma kwa mwaka 2023/24 (Health Promotion Annual Work Plan) na kuainisha vyanzo vya fedha za utekelezaji wa afua za kipaumbele. 

Kikao kazi hiki kilianza tarehe 13, Februari 2023 na kitaendelea hadi tarehe 17, Februari 2023 ambapo washiriki waliohudhuria ni kutoka Wizara ya Afya, OR-TAMISEMI, wawakilisi wa Wadau mbalimbali.

Imeelezwa kuwa, baada ya kikao kazi hicho kitaleta mabadiliko katika utekelezaji wa afua mbalimbali za afya, miongoni mwa Wadau waliohudhuria katika kikao kazi ni pamoja na mwakilishi kutoka Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani(UNICEF], PSI, USAID, PACT, TCDC, SIKIKA, D-Tree, Marie Stopes, World Vision, Save the Children, TRCS, EGPAF, AMERICARES, Mkapa Foundation, Girl Effect Apotheker, na T-Marc Tanzania.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)