DKT. DUGANGE AANZA ZIARA MKOA MANYARA

MUUNGANO   MEDIA
0


Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange( Mb) leo tarehe 20 Februari 2023 amewasili Mkoani Manyara na atakuwa na ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu ya barabara ikiwa ni pamoja na Ukusanyaji wa Mapato na Utoaji wa mikopo ya 10% katika Halmashauri.

DKt. Dugange leo atafanya ziara katika halmashauri ya Wilaya ya Babati ambapo atatembelea na kukagua Hospitali ya Wilaya Babati, Ujenzi wa shule ya sekondari Sarame, ukaguzi wa Barabara ya Magugu - Kisangaji na kituo cha afya Gallapo.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)