CHAGUZI ZA MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI NGAZI ZA MIKOA UKOMO TAREHE 1, MACHI 2023.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amemuagiza Mkurugenzi msaidizi Wa Maendeleo ya Jinsia Bi Rennie Gondwe kuhakikisha Mikoa yote ambayo haijafanya uchaguzi wa majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ngazi ya mkoa kufanya hivyo kabla ya tarehe mosi mwezi Machi mwaka 2023.

Wakili Mpanju ametoa agizo hilo wakati akifungua mkutano wa uchaguzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoani Arusha na kubainisha kuwa hadi sasa ni mikoa 16 kati ya 26 ndio imeshafanya chaguzi zake hali inayopelekea ucheleweshwaji wa uzinduzi wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi la kitaifa.

Wakili Mpanju anasema katika kila mkoa ni lazima liwepo jukwaa ambalo wanawake watakutana kujadili ajenda zao na namna ya kuzifikia fursa mbalimbali za kiuchumi na kielimu ili kuweza kukua kiuchumi.

 "Nikuagize Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya jinsia, hakikisheni mikoa yote ambayo haijafanya chaguzi za ngazi za mikoa, mikoa yote 26 ya Tanzania bara mpaka ifikapo mwisho wa mwezi wa pili hakikisheni wawe wameshafanya uchaguzi wa uwezeshaji wanawake kiuchumi ngazi ya Mikoa mabla ya mwezi Machi mwaka 2023" amesema Mpanju.

Wakili Mpanju akatumia fursa hiyo kuwasisitiza wale ambao watachaguliwa kuongoza majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa ngazi za mikoa kuhakikisha wanakua mwangaza wa kuzivumbua fursa mbalimbali zitakazo wanufaisha wanawake kiuchumi.


"Nia ya serikali ni hayo majukwaa yatumike kuwakutanisha na watoa huduma mbalimbali wanaohitajika katika kuwawezesheni nyinyi kufanya shughuli zenu za kiuchumi, muweze kujua fursa gani za kiuchumi zipo ili muweze kuzifikia na kukuza kipato chenu na taifa kwa ujumla" amesema Mpanju


Aidha Wakili Mpanju anasema nia ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kila mtu ashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa taifa letu.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)