Na.Faustine Gimu Galafoni
Katika kuadhimisha siku ya
wanawake wa Kiadventista ya Maombi
Duniani,Washiriki wa kanisa la Waadventista Wasabato wameaswa kuongeza juhudi kufanya maombi kwa ajili ya kuiombea dunia
hasa katika kipindi hiki kigumu cha siku
za mwisho zilizojaa wasiwasi,maasi na vita.
Hayo yalibainishwa Mwishoni mwa Juma lililopita na
baadhi ya akina mama kutoka kanisa la Waadventista Wasabato Chang’ombe Dodoma
wakati wakifanya mahojiano maalum na mtandao huu mara baada ya
kufanyika ibaada ya Sabato kanisani hapo.
Beth Swai,mkurugenzi idara ya wana
wa kike Kanisa la Waadventista Wasabato Chang’ombe Cecilia Kisaka ,pamoja na Haika
Joas ni miongoni mwa wanawake na washiriki wa kanisa la Waadventista Wasabato
Chang’ombe walisema katika kuadhimisha
siku ya maombi kwa wana wa kike ,kwa kumtazama Nabii Yoshua kama mtumishi wa
mungu ,mcheshi ,msafi na mwenye ucha Mungu inapaswa kila mkristo kuwa na
upatanisho katika maombi.
“Tumeona Yoshua
alivyosimama katika maombi hakutetereka hivyo na sisi kama washiriki tunapaswa
kusimama imara katika maombi,hivyo katika maombi hakuna kuchoka ni wakati wa kusonga mbele”alisema mmoja wa akina mama hao.
Aidha,mkurugenzi idara ya wana wa
kike Kanisa la Waadventista Wasabato Chang’ombe Dodoma Cecilia Kisaka alisema katika
kuadhimisha siku ya maombi ya kimataifa ya wana wa kike waliandaa program mbalimbali
katika kanisa hilo zikiwemo programu za mahubiri,pamoja na ibaada za nyimbo kwa
wanawake.
Akihubiri katika siku ya kimataifa
ya wanawake ya maombi kanisa la
Waadventista Wasabato Chang’ombe mkurugenzi idara ya watoto kanisani hapo
Jackline Masikini amekazia kwa kila mwumini kuwa karibu na uhusiano na
Mungu.
Akibainisha kupitia somo
lililokwenda na kichwa kisemacho”Kuomba katika siku za mwisho Cecilia alisema mwanadamu anaweza kuzungumza
na Mungu endapo ataweka mahitaji yake na maombi hutunza kumbukumbu huku akinukuu kitabu cha Yoshua 5:13 jinsi Yoshua
alipokuwa karibu na mji wa Yeriko na alivyokuwa jasiri katika maombi na
kukabiliana na changamoto zilizomkabili.
Sisi sote tunatakiwa kuwa karibu na Mungu kwa njia ya maombi kwani
tutakuza uhusiano wetu na mungu,tutaondoa hofu zinazotawala hasa katika maisha
yetu ya leo, na kukuza kumbukumbu zetu kupitia maombi,kwani yanaweza hata
kubadili na kurahishisha hata jambo lisilowezekana”alisema.
Mkurugenzi idara ya watoto
kanisa la Waadventista Wasabato Chang’ombe Jackline Masikini akitoa huduma ya mahubiri
katika siku ya kimataifa ya wanawake ya maombi kwa kanisa la Waadventista
Wasabato Ulimwenguni.
Akitoa neno katika ibaada ya watoto
kanisa la Waadventista Wasabato Chang’ombe , ELLEN LUPIA aliwaasa watoto kuwa watii kwa wazazi wao na kuhakikisha wanaenda katika
mienendo mizuri kwani inaepusha wizi na vifungo visivyo vya lazima.
“Watoto tunapaswa kuwa na tabia
njema ,mnajua wizi ni mbaya ,hivyo mara nyingi mtoto anayekuwa na tabia mbovu
ni yule asiyekuwa na utii kwa wazazi na tabia ya udokozi huanza polepole “alisema.
Ellen Lupia akihubiri katika ibaada ya watoto
katika kanisa la Waadventista Wasabato Chang’ombe jijini Dodoma .
MWISHO.