VIKOSI VYA URUSI VYAUTEKA MTAMBO YA NISHATI YA NYUKLIA WA UKRAINE

0

 


Vikosi vya Urusi vimekiteka kinu kikubwa cha nyuklia barani Ulaya mapema leo, kufuatia mapambano na jeshi la Ukraine, ambayo yalisababisha moto na hofu ya kulipuka kwa mtambo huo. 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy, amesema Ulaya inapaswa kuamka sasa kufuatia moto huo. "Watu wa Ulaya, tafadhali amkeni. Waambieni wanasiasa wenu - Wanajeshi wa Urusi wanashambulia mtambo wa nyuklia Ukraine. Mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhia. mjini Enerhodar. Kuna vinu sita vya nyuklia huko - sita! Chernobyl ilikuwa mtambo mmoja ambao ulilipuka,"alisema Zelenskiy. Maafisa wa Ukraine wamesema moto huo umezimwa na hakujabainika uvujaji wowote wa miale ya nyuklia. 

Mtambo huo wa umeme upo kusini mwa Ukraine, kwenye Mto Dnipro, na uzalisha humusi moja ya umeme wa Ukraine. 

Moto wowote karibu na mtambo wa nyuklia unarejesha kumbukumbu ya janga la Chernobyl la mwaka 1986, pia nchini Ukraine, ambalo lilisababisha vifo vya mamia ya watu na kusambaza uchafuzi wa miale kote barani Ulaya.


Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)