Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu[Kazi ajira,vijana ,na wenye ulemavu]Prof.Joyce Ndalichako.
Na.Faustine
Gimu Galafoni,Dodoma.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu[Kazi ajira,vijana ,na wenye ulemavu]Prof.Joyce
Ndalichako amepiga marufuku kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini tabia ya kuwaweka ndani[kortini]
watumishi wa umma wenye makosa yasiyo ya jinai.
Prof.Ndalichako
amepiga marufuku hiyo leo Machi 12,2022 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano
wa baraza kuu la
shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania[TUCTA] ambapo amesema haipaswi kuwekwa ndani
watumishi wa umma kwa makossa yasiyo ya jinai kwani pamekuwa na tabia ya wakuu
wa wilaya na wakuu wa mikoa kuwaweka ndani watumishi wa umma kwa makossa yasiyo
ya jinai.
Baadhi ya wanawake kamati ya wanawake shirikikisho la vyama wafanyakazi[TUCTA]wakimpokea kwa shangwe ,Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu[Kazi ajira,vijana ,na wenye ulemavu]Prof.Joyce Ndalichako .
Hivyo,amesema
makosa ya kiutendaji kwa watumishi yachukuliwe hatua sehemu za kazi.
"Hilo suala la kuwaweka ndani watumishi kwa makosa yasiyo ya jinai ,niendelee kuwakubusha waendelee kufuata miongozo iliyowekwa "amesema.
Aidha,Prof.Ndalichako
amewaagiza waajiri wote nchini kuhakikisha vikao vya mabaraza ya wafanyakazi
vifanyike kwa mujibu wa matakwa ya kisheria ikiwemo kulipa posho stahiki kwa
wafanyakazi.
"Nichukue nafasi hii kuyaagiza mabaraza ya wafanyakazi yafanyike kwa mujibu wa sheria"amesema.
Rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania[TUCTA] Tumaini Nyamhokya amesema kuna haja kwa serikali kutekeleza ipasavyo kuwarejesha kazini watumishi wa darasa la saba kwani kuna baadhi ya taasisi zimekuwa zikiwakataa na kuwanyima stahiki zao .
Baadhi ya washiriki mkutano wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi[TUCTA]wakifuatilia wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa katika mkutano huo jijini Dodoma.
"Kama alivyosema Rais ,suala la kuwarejesha kazini wa darasa la saba ,nalo linapaswa kuangaliwa upya kwa sababu sio makosa yao"alisisitiza.
Rais wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania[TUCTA] Tumaini Nyamhokya
Mwenyekiti wa kamati ya wanawake wa shirikisho hilo Rehema Ludanga amesema kuwa bado kuna changamoto ya utekelezaji wa sheria ya mkataba wa kazi.
Mwenyekiti wa kamati ya wanawake wa shirikisho hilo Rehema Ludanga.
"Changamoto kubwa tunazokabiliana nazo mpaka sasa hivi kuna baadhi ya maeneo bado utekelezaji wa sheria hauko sawasawa "amesema.