Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo na watendaji wa Bohari ya Dawa (MSD) wakati Kamati hiyo ilipokagua kiwanda cha kutengeneza barakoa, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Brig.Jen.Dkt. Gabriel Mhidize, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekhalage Na kulia ni Katibu wa Kamati Erick Maseke
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Dawa cha Keko, Betia Kaema akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jinsi dawa zinavyotengenezwa wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bohari ya Dawa (MSD) na kukagua kiwanda hicho na Kiwanda cha kutengeneza barakoa.
Afisa Udhibiti Ubora kutoka Bohari ya Dawa (MSD), akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jinsi mashine ya kutengeneza barakoa inavyofanya kazi wakati Kamati hiyo ilipotembelea MSD na kukagua kiwanda hicho na Kiwanda cha kutengeneza dawa cha Keko.