WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amesema wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne mwaka 2021 wanayo nafasi ya kubadili machaguo ya tahasusi (Combination) na kozi mbalimbali wanazohitaji kusoma kulingana na ufaulu wao.
Kauli hiyo ameitoa
leo Machi 29,2022 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari
Waziri Bashungwa amesema, hatua hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi
waliohitimu Kidato cha Nne kutokujaza fomu (Selfom) kwa uhakika wakati wanachagua
combination zau kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika
masomo yao.
“Ofisi ya Rais
-TAMISEMI imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzi data taarifa
zilizo kwenye fomu za mwanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni,
hii inazoa nafasi kwa wanafunzi kuweza kufanya mabadiliko ya machaguo yao”
amesema Bashungwa
Aidha amesema kuwa
Serikali imetoa fursa kwa wahitimu wa Kidato cha Nne kubadili machaguo yao ili
kutoa nafasi zaidi kwa mwanafunzi kusoma tahasusi au kozi itakayomwandaa kuwa
na utaalam ambao unaendana na machaguo yake hapo baadae.
“Amewataka wazazi
kushiriki kikamilifu na kukubaliana na mwanafunzi katika zoezi hili ili
pasiwepo na malalamaiko yoyote ya mwanafunzi kuwa amepangiwa machaguo ambayo
hakuyachagua hapo baadae” amesema Waziri Bashungwa
Hata hivyo
amefafanua kuwa zoezi la kubadilisha tahasusi kwa mwanafunzi linafanyika kwa
utaratibu wa kuingia kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi (student Selection
MIS) kupitia kiunganishi cha selform.tamisemi.go.tz kwa kutumia namba ya
mtihani.
Waziri Bashungwa
ametoa ushauri kwa wazazi,walezi na wanfunzi kuendelea kutumia dawati la huduma
kwa wateja kupitia barua pepe helpdesk@tamisemi.go.tz au na kituo cha
huduma kwa wateja kwa simu namba +255 262 160 20 na +255 735 260 210 au fika
katika ofisi za Mamlaka za Serikali za Mitaa.