Tazama Hapa Picha za Tundu Lissu Alivyowasili na Kupokelewa Ubelgiji
Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amewasili katika uwanja wa
ndege jijini Brussels, nchini Ubelgiji ambapo amepelekwa kwa ajili ya
awamu ya tatu ya matibabu yake yatakayohusisha mazoezi ya viungo.
Tundu Lissu amewasili jijini hapo akitokea katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu kwa muda wa takribani miezi minne sasa, kutokana na kushambuliwa kwa risasi.
Mbunge
Tundu Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni,
alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana, alipokuwa akitokea
Bungeni, majira ya saa 7 mchana, karibu na nyumbani kwake Area D, Mjini
Dodoma.
Kwa
Mujibu wa taarifa ya madaktari waliokuwa wanamtibu, walieleza kuwa
jumla ya risasi 16 zilimpata Tundu Lissu mwilini mwake, na wamefanikiwa
kuzitoa, isipokuwa moja ambayo iko nyuma ya uti wa mgongo wake.
Tundu
Lissu alieleza kuwa wataalamu na madaktari wake walishauri kuwa risasi
hiyo ni hatari zaidi kama ikitolewa kuliko ikibaki ndani ya mwili wake,
kutokana na eneo ilipokwama.
==>Picha za Mbunge Tundu lissu alipowasili jijini Brussels kwa ajili ya matibabu zaidi.