NA FAUSTINE GIMU GALAFONI KAHAMA
Tamasha la Mafunzo na Michezo kwa watoto waliochini ya miaka 16 la Kanisa La TAG Mavuno Mhungula Kahama lililoanza Disemba 28 ,2017 Limehitimishwa hapo jana Katika uwanja wa shule ya sekondari OASIS.
Katika Tamasha hilo lililoandaliwa na mchungaji wa kanisa la TAG Mavuno Emanuel Gewe,Timu zilizofanikiwa kuingia nusu fainali ni Samaria na Philips ambapo katika mchezo wa jana dakika zote 90 zilitoka kwa kufungana 2 kwa 2 .
Timu ya Msamaria goli la kwanza lilifungwa na Doto Sadoki na la pili likifungwa na Kulwa Robert.
Katika timu ya Philips ,bao la kwanza lilifungwa na Juma Said na la pili likipachikwa na Mdagije Morice.
Baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa kutoka 2kwa 2 hatimaye ziliingia kwenye matuta ambapo kwa upande wa timu ya Samaria Penalt ya kwanza ilifungwa na Yusuf Lukas ya pili ikifungwa na Kulwa Robert .Kwa upande wa Philips Penalt ilifungwa na Juma Said.
Kwa hali hiyo Samaria iliibuka kuwa mshindi wa mabao 2 kwa 1.
Katika mashindano hayo timu zilizofanikiwa kuingia Fainali ni Sinai na Efeso ambapo Sinai waliibuka kuwa vinara kwa goli 2 kwa 1 dhidi ya Efeso.
Kwa timu ya Sinai,goli la kwanza lilifungwa na Charles Joseph na la pili likipachikwa na Said Mbwende huku kwa upande wa Efeso goli likifungwa na Paulo Simon.Kwa hali hiyo Sinai ilibuka kuwa kinara kwa mashindano hayo kwa upande wa wavulana na Katika timu ya mpira wa pete ya wasichana Efeso walikuwa wa kwanza.
Mfungaji bora katika tamasha hilo kwa wanaume ni Said Mbwende timu ya Sinai,Mchezaji bora ni Simon Lazaro timu ya Efeso na mchezaji mwenye nidhamu ni Kassim Hamza timu ya sinai .
Kwa upande wa wasichana ni mfungaji bora ni Lusi Masele Timu ya Philip ,mchezaji bora ni Janet Richard timu ya Philip na mchezaji mwenye nidhamu ni Advera Musa timu ya Efeso.
Mwandaaji wa mashindano hayo Mchungaji wa kanisa la T.AG.Mavuno la Mhungula Kahama,Emanuel Gewe lengo la Tamasha hilo la watoto ni kuwaimarisha watoto kiafya ,kujenga mahusiano na ukaribu pamoja na kuwafurahisha kwani furaha kubwa kwa watoto ni michezo.
Gimu Blog ilipata fursa ya kuzungumza na baadhi ya watoto na wachezaji hao ambapo wamewaomba wadau wa michezo wengine kuangalia vipaji vya watoto makanisani huku wakimpongeza mwandaaji wa Tamasha hilo Mchungaji wa Kanisa la T.A.G Mavuno lililopo Mhungula Kahama Emanuel Gewe.
Makocha wa timu hizo Kulwa Salum kutoka timu ya Wasamaria,Musa Salum timu ya Philips,Kornelio Joel wa timu ya Sinai na Richard Bernad kutoka timu ya Efeso walisema kuwa Tamasha hilo limewapa moyo wa kuendelea kuinua vipaji vya watoto na wataendelea kujipambanua zaidi.