Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo ya kunyesha kwa mvua
kubwa katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia leo Alhamisi na kesho
Ijumaa.
Taarifa
ya TMA imebainisha mikoa itakayokubwa na mvua hizo ni Pwani ya Kusini
ambayo ni Lindi na Mtwara, Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni
Mbeya, Iringa, Songwe na Rukwa, Dar es Salaam na Pwani.
“Upepo
wa Pwani, unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini; kwa kasi ya Km 30 kwa
saa kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya
Kusini,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza;
“Hali
ya Bahari, inatarajiwa kuwa mawimbi madogo hadi makubwa kiasi na
matazamio kwa siku ya Ijumaa Januari 5,2018, kuongezeka kwa mvua katika
mwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi.”
Hata
hivyo, tayari mvua hizo zimekwisha kuanza na mikoa ya Dar es Salaam na
Pwani mvua ilinyesha jana Jumatano usiku katika maeneo mbalimbali ya
mikoa hiyo.