PICHA KUTOKA MAKTABA
Imeelezwa kuwa jumla ya
watoto 400 katika halmashauri ya mji wa Kahama wamekamatwa wakisafirishwa ndani
na nje ya nchi katika kipindi cha mwezi januari hadi desemba kwa lengo la
kupelekwa kufanya kazi katika maeneo mbali mbali.
Hayo yamebainishwa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
yaliyoadhimishwa katika bwalo la polisi mjini kahama.
Akisoma taarifa ya
halmashauri afisa maendeleo ya jamii kutoka katika hamashauri ya mji wa
Kahama Marry Chima amesema kuwa jumla ya
watoto 400 wamekamatwa wakisafirishwa kutoka katika maeneo mbalimbali ndani na
nje ya nchi ambapo amesema watoto 360 ni kutoka nchini Burundi watoto 20 kutoka
Rwanda na wengine 20 wakitoka chini hapa katika maeneo ya Ngara na Kigoma.
Ameongeza kuwa katika
kuendelea kupambana na suala la ukatili wa kijinsia nchini watoto 27 wamelazimika kukatisha
masomo baada ya kubainika kuwa na ujauzito jambo ambalo linakatisha ndoto zao
na linapaswa kukemewa kwa nguvu zote.
Naye mwenyekiti wa
halmashauri ya mji wa Kahama bw, Abel Shija ambaye alikuwa mgeni rasimi katika
maadhimisho hayo amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na taasisi mashirika na
wadau mbalimbali wanapashwa kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kwani ndio
msingi utakaowezesha kutokomeza ukatili katika jamii.
Maadhimisho ya ukatili
a kijinsia hufanyika kila mwaka ifikapo novemba 25 hadi disemba 10 ambapo leo
kilele cha maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa bwalo la polisi mjini
kahama huku kauli mbiu isemayo ukatili dhidi ya wanawake na watoto
hautomuacha mtu salama ,chukua hatua pinga ukatili.
mwisho