Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 28 Desemba, 2017 amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu
rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasilisha fomu hiyo Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017.
“Mhe.
Jaji Nsekela ikifika tarehe 31 Desemba, ambayo ni siku ya mwisho kwa
Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone
sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” amesisistiza Mhe. Rais Magufuli.
Kwa
upande wake Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela amemshukuru na kumpongeza
Mhe. Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu
kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi
wa umma sio ombi.
“Viongozi
hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo
tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo na kuna sababu
zake za msingi” amesema Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela.
Aidha,
Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa
kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki sambamba na tamko hilo, na
amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine.
Tamko
la viongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni linatolewa kwa mujibu
wa kifungu cha 9 na cha 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma
namba 13 ya mwaka 1995.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli
akiwasili Katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma
Jijini Dar Es Salaam kuwasilisha fomu zake za tamko la Rasilimali na
madeni kwa Viongozi wa Umma Disemba 28,2017.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli
akisalimiana na Kamishina wa Maadili Jaji Mstaafu Haroild Nsekela
alipowasili Katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma
Jijini Dar Es Salaam kuwasilisha fomu zake za tamko la Rasilimali na
madeni kwa Viongozi wa Umma Disemba 28,2017.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Katika Ofisi Za Sekretarieti
Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma Jijini Dar Es Salaam kuwasilisha fomu
zake za tamko la Rasilimali na madeni kwa Viongozi wa Umma Disemba
28,2017.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli
akihakiki fomu zake kabla ya kuziwasilisha kwa Kamishina wa Maadili Jaji
Mstaafu Haroild Nsekela Katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya
Viongozi Wa Umma Jijini Dar Es Salaam Disemba 28,2017.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli
akimsikiliza Kamishina wa Maadili Jaji Mstaafu Haroild Nsekela mara
baada ya kuwasilisha fomu zake za tamko la Rasilimali na madeni kwa
Viongozi wa Umma Katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa
Umma Jijini Dar Es Salaam Disemba 28,2017.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli
akimshukuru Kamishina wa Maadili Jaji Mstaafu Haroild Nsekela mara baada
ya kuwasilisha fomu zake za tamko la Rasilimali na madeni kwa Viongozi
wa Umma katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa Umma
Jijini Dar Es Salaam Disemba 28,2017.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Kamishina wa Maadili Jaji Mstaafu Haroild Nsekela wakiangalia
moja ya ofisi za Serikali zilizopo katika jengo la Sukari House mara
baada ya kuwasilisha fomu zake za tamko la Rasilimali na madeni kwa
Viongozi wa Umma katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa
Umma Jijini Dar Es Salaam Disemba 28,2017.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli
akisindikizwa na Kamishina wa Maadili Jaji Mstaafu Haroild Nsekela
wakiangalia moja ya ofisi za Serikali zilizopo katika jengo la Sukari
House mara baada ya kuwasilisha fomu zake za tamko la Rasilimali na
madeni kwa Viongozi wa Umma katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya
Viongozi Wa Umma Jijini Dar Es Salaam Disemba 28,2017.
Rais
Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli
akiwapungia mkono Wananchi waliokuwepo nje ya jengo la Sukari House mara
baada ya kuwasilisha fomu zake za tamko la Rasilimali na madeni kwa
Viongozi wa Umma katika Ofisi Za Sekretarieti Ya Maadili Ya Viongozi Wa
Umma Jijini Dar Es Salaam Disemba 28,2017.Disemba 28,2017.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Desemba, 2017