Katika kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho
wa mwaka,vitendo vya wizi katika kijiji cha sungamile halmashauri ya Msalala
wilayani Kahama Mkoani shinyanga vimeongezeka baada ya wahalifu kuanza kuvamia
kaya hadi kaya pamoja na maduka na
kupora mali mbalimbali.
mwenyekiti wa kijiji cha Sungamile Ngusa
Mayunga amesema kuwa matukio ya wizi katika kijiji hicho yamekithiri
likiwemo na tukio la majambazi kutembea mtaa kwa mtaa na kuomba pesa kwa lazima
huku wakitumia bunduki kwa kutishia.
Siku ya kwanza waliiba zaidi ya shilingi
milioni moja na laki 7 ambapo walikuwa wanadai kwa nguvu.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa mara
baada ya siku moja kupita duka moja mali ya Mfanyabiashara aliyejulikana kwa
jina moja la Mashaka liliporwa vitu mbalimbali vikiwemo simu za mkononi
6,mafuta ya kupikia ,sukari pamoja na
vocha.
Katibu wa muda wa wafanyabiashara wa kijiji hicho Nzego Mihambo
ametaja thamani ya vitu vilivyoibiwa ambapo ni zaidi ya shilingi laki saba.
Nao wananchi wa kijiji cha sungamile
wamezungumzia kutokana na vitendo vya uhalifu kukithiri kijijini hapo huku
wakiiomba serikali kuimarisha ulinzi na usalama ili kutokomeza vitendo vya
wizi.
Hivyo kutokana na tukio hilo la kuporwa
duka ambalo limetokea usiku wa kuamkia
jana jeshi la jadi sungusungu sungamile
liliamuru mlinzi aliyekuwa katika zamu Shangalile Elisha kulipa fidia zote bila kujali katiba ya umoja
wa wafanyabiashara wa kijiji hicho ambapo inasema kuwa pindi panapotokea
hitilafu wenye wajibu wa kulipa ni walinzi wote.
Na.Faustine Gimu Galafoni.