SERIKALI YAELEZA MKAKATI WAKE KUPANDISHA HADHI MWANZA AIRPORT.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Na Avelina Musa - DODOMA.


Serikali imeeleza mpango wa kuimarisha miundombinu ya viwanja vya ndege nchini kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), hatua inayolenga kuboresha huduma za usafiri wa anga na kuchochea uchumi wa Nchi.


 Hayo yamesemwa na Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa  Bungeni Jijini Dodoma wakati  akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi 2026/2027 ambapo amesema Serikali imepanga kupandisha hadhi Kiwanja cha Ndege cha Mwanza na kukifanya kuwa cha Kimataifa.


 Prof.Mbarawa amesema tayari usanifu na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa jengo jipya la abiria umekamilika, litakaloweza kuhudumia hadi abiria milioni 2.5 kwa mwaka.


 "Maboresho yanaendelea katika Kiwanja cha Ndege cha Arusha, ikiwemo mfumo wa taa za kuongozea ndege uliofikia asilimia 65, hatua inayoongeza uwezo wa huduma hata nyakati za usiku"Amesema.


Aidha amesema Serikali inaendelea kuboresha viwanja vya ndege ili Tanzania iwe kitovu muhimu cha usafiri wa anga Afrika Mashariki.





Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)