WIZARA YA AFYA KUIMARISHA MAFUNZO YA UFUATILIAJI WA USALAMA WA MAJI KWA WATAALAMU WA AFYA MAZINGIRA MIPAKANI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 



Wizara ya Afya kupitia Sehemu ya Afya Mazingira kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), imeendesha mafunzo maalum ya ufuatiliaji wa usalama wa maji kwa wataalamu wa afya mazingira kutoka halmashauri pamoja na vituo vya afya vilivyopo mipakani mwa nchi.

‎Mafunzo hayo Yameanza kufanyika leo mkoani Morogoro, yamelenga kuimarisha uwezo wa wataalamu hao katika kusimamia na kufuatilia ubora na usalama wa maji yanayotumika katika vituo vya afya mipakani, pamoja na maeneo yanayozunguka mipaka. 


‎Hatua hii inalenga kuhakikisha huduma za afya zinatolewa katika mazingira salama na yenye kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa vya usafi na usalama wa maji.

‎Kupitia mafunzo hayo, washiriki wamejengewa uwezo wa kutambua vihatarishi vinavyoweza kuathiri ubora wa maji, kufanya tathmini ya mifumo ya usambazaji maji, kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa maabara, pamoja na kuweka na kutekeleza mipango ya usalama wa maji.

‎mafunzo yamehusisha mbinu za ufuatiliaji endelevu na utoaji wa taarifa kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka pale changamoto zinapojitokeza.

Aidha wataalam hao waliopewa mafunzo watahusika pia katika kutoa elimu ya afya kuhusu usalama wa maji kwa jamii zinazozunguka mipakani ili kuwawezesha kujikinga dhidi ya magonjwa yanayotokana na kunywa maji yasiyo salama.



Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)