Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kutumia fursa ya Maadhimisho ya wiki ya Magonjwa Yasiyoambukiza kupima afya bila malipo.
Mhe.Shekimweri ametoa wito huo mara baada ya kutembelea mabanda mbalimbali yanayotoa huduma za afya bila malipo katika viwanja vya Nyerere Square Dodoma ikiwa ni katika maadhimisho ya Magonjwa Yasiyoambukiza ambapo huduma hizo zinatolewa hali tarehe 14,Novemba,2025.
Aidha, Mhe.Shekimweri amesema njia sahihi ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na kubadili mtindo wa maisha ikiwemo ulaji sahihi na kufanya mazoezi mara kwa mara.
Wiki ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza 2025 inakwenda sambamba na Kaulimbiu isemayo "Chukua Hatua, Dhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza" ambapo Halmashauri,Wilaya na Mikoa imekuwa ikiadhimisha kwa kutoa huduma mbalimbali za afya katika maeneo yao.
Mwisho.

